Header Ads Widget

WANANCHI WA KIJIJI CHA ULIWA NJOMBE WAVUTANA JUU YA MRADI WAO WA MAJI KUZINDULIWA NA CHADEMA

 






Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAAP NJOMBE


Wakati Chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA kanda ya Nyasa na mkoa wa Njombe wakizindua mradi wa maji katika kijiji cha Uliwa halmashauri ya mji wa Njombe unaotajwa kujengwa na wananchi kwa kushirikiana na viongozi wa Chadema,Baadhi ya wananchi wasio na vyama pamoja wale wa CCM wamelalamikia hatua ya Chadema kuzindua mradi huo.


Wakizungumza mbele ya Uongozi wa Wakala wa maji vijijini Ruwasa wilaya ya Njombe na viongozi ngazi ya kijiji na Kata ya Iwungilo waliofika kusikiliza malalamiko hayo baadhi ya wakazi hao akiwemo Valelia Manga,Emelda Mtewele na Salvius Mwalongo ambaye ni mwenyekiti wa kijiji cha Uliwa ambaye naye alichangia takribani shilingi laki mbili ujenzi wa mradi huo wanasema hawakukubaliana nani atauzindua walishangaa kuona Chadema wanauzindua pasina makubaliano ya pande zote.


Wengine akiwemo Sigfrid Msigwa,Longnus Mlowe na Casmiry Mgina mwenyekiti wa kamati ya ukusanyaji michango ya ujenzi wa mradi huo wamesema hawaoni sababu ya malumbano kwa kuwa wametaabika kwa kukosa maji safi Tangu mwaka 1976 hivyo viongozi wa serikali ngazi ya kijiji wanapaswa kuketi katika meza ya pamoja kuliweka sawa jambo hilo kwani hata Viongozi wa Chadema waliozindua mradi huo waliwachangia kiasi cha shilingi laki Nane kwa ajili ya kuendeleza mradi huo.


Aidha Afisa mtendaji wa Kijiji cha Uliwa Stunisius Mlowe amesema hajawahi kupata taarifa ya uwepo wa mradi huo licha ya mwenyekiti wa kijiji kuchangia ujenzi huo huku akiwataka wananchi kuzingatia sheria za nchi katika utekelezaji wa miradi mbalimbali.


Kwa upande wake Kaimu meneja wa Ruwasa wilaya ya Njombe Bakari Kitogota amesema kwa kuwa wananchi wamefikisha maji katika vitongoji viwili vya Itowa na Kanada wao watafanya mpango wa kupeleka maji hayo katika vitongoji viwili vilivyosalia ambavyo vyote vinategemea chanzo kimoja na kwamba kama wakala watakwenda kupima maji hayo.


Germanus Ndumbaro Afisa mtendaji wa kata ya Iwungilo amesema hakuwa na taarifa ya uzinduzi wa mradi wa maji katika kijiji hicho zaidi ya kupokea barua ya uwepo wa mkutano wa Hadhara wa CHADEMA jambo ambalo walikiuka taratibu kwa mujibu wa barua yao.


Mkaguzi msaidizi wa Polisi ambaye ni mkuu wa kituo cha Polisi Uwemba Afande Teddy Kossam amesema kila mmoja anapaswa kuishi kwa amani bila kufanyiana vurugu kwa kuwa nchi yetu imeruhusu mfumo wa vyama vingi na kwamba Malumbano ya kisiasa yaliyopo yanapaswa kuisha.


Mradi huo wa maji uliozinduliwa Mei 19,2023 na mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Nyasa Mchungaji Peter Msigwa umetajwa kugharimu kiasi cha shilingi milioni 12 na umeanza kutoa huduma kwa wakazi 150 huku wananchi zaidi ya 400 wakiendelea kukosa maji.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS