Header Ads Widget

WAFANYABIASHARA WATAKIWA KUTOA MAONI YAO KWA KAMATI YA WAZIRI MKUU

 



Na Fadhili Abdallah,Kigoma



TUME ya Waziri mkuu kassim Majaliwa ya kukusanya maoni kuhusu changamoto zinazowakabili wafanyabiashara nchini imewataka wafanyabiashara nchini kutoa maoni yao kwa wajumbe wa tume hiyo bila kuogopa na maoni hayo yatafikia viongozi wa serikali kama yalivyotolewa ili yafanyiwe kazi.


 

Mjumbe wa tume hiyo  wa tume hiyo anayesimamia  ukusanyaji maoni kwa mikoa ya Magharibi na kanda ya ziwa, Reheme Madenge alisema kuwa wafanyabisahara wa mkoa Kigoma wanapaaswa waiamini tume hiyo kwani maoni yao yatafanyiwa kazi kikamilifu.




Akizungumza kabla ya kuhitimisha kikao hicho Madenge alisema kuwa maoni hayo yaliyotolewa na wafanyabiashara yatawasilishwa kwa Waziri Mkuu kama maelekezo yalivyotolewa na kwamba mpango huo unasimamiwa na serikali kuwezesha kuondoa kero lakini kuwafanya wafanyabiashara hao kufanya shughuli zao kwa tija.



Katika mkutano huo uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano ofisi ya Mkuu wa mkoa Kigoma wafanyabiashara hao wameinyooshia kidole Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) wakitaka ifanye kazi zake kwa kusimamia kodi na tozo ambazo ni rafiki kwa wafanyabiashara.

 

Mmoja wa wafanyabiashara hao, Brian William Wakala wa forodha katika bandari ya Kigoma alisema kuwa utitiri wa kodi na tozo umekuwa changamoto kubwa kwao kwani kodi ya upakiaji na upakuaji wa shehena imekuwa kubwa kwa bandari ya Kigoma ukilinganisha bei ya chini kwa bandari ya Dar es Salaam.



Alisema kuwa hali hiyo imefanya wafanyabiashara wa Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo kusafirishia shehena zao kupitia bandari ya Mpulungu Zambia ambayo inatoka dola 65 kwa kontena ukilinganisha na dola 140 kwa bandari ya Kigoma.

 

Naye Mfanyabiashara wa gesi, Issa Mangapi alisema kuwa kodi na Tozo za TRA na manispaa zimekuwa kero kubwa kwa wafanyabiashara ikiwemo kodi ya huduma (Service Levy) ambayo ametaka iondolewe huku akiitaka serikali itumie wataalam wake kufanya utafiti wa kodi na tozo ambazo ni kero kwa wafanyabiashara.



Francis Kabula Mwenyekiti wa wavuvi katika ziwa Tanganyika ameitaka serikali kuangalia kodi na tozo zinazotozwa kwenye maboti ya usafirishaji na mtumbwi ya uvuvi kwani haziendani na kazi zinazofanywa na wenye maboti yao.

 


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI