NA WILLIUM PAUL, MOSHI.
WANAWAKE mkoani Kilimanjaro wameshauri kujikita katika swala la malezi dhidi ya watoto ili kupambana na matukio ya ukatili dhidi yao ambayo yamekuwa yakishamiri.
Kauli hiyo imetolea na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake (UWT) mkoa wa Kilimanjaro, Wakili Msomi Elizabeth Minde akitoa mafunzo na Elimu ya Unyanyasi wa kijinsia, malezi na makuzi ya watoto kwa Wenyeviti UWT Wilaya, Makatibu UWT Wilaya na Madiwani viti maalum.
Wakili Elizabeth alisema kuwa, kumekuwa na matukio mbalimbali ya ukatili dhidi ya watoto ambapo yamekuwa yakichangiwa na kiasi kikubwa kwa Wazazi hasa wakinamama kuwa bize na shughuli zao na kusahau jukumu la malezi.
"Wakinamama tumekuwa buzi sana katika kutafuta hela na kusahau kuwa tunawajibu mkubwa wa kusimamia na kushughulikia swala la malezi la watoto wetu hali ambayo imekuwa ikichangia kufanyika kwa matukio mbalimbali ya ukatili dhidi ya watoto tunapaswa kubadilika na kutambua jukumu letu katika jamii" alisema Wakili Elizabeth.
Mwenyekiti huyo alitumia pia nafasi hiyo kuwataka viongozi kuubiri swala la malezi katika jamii kwani sio swala la walimu pekee bali kila mzazi anawajibika katika swala la kulea.
Kwa upande wake Katibu wa Chama cha Mapinduzi manispaa ya Moshi, Ibrahim Mjanakheri aliwataka wakinamama kutembea kifua mbele na kuzitangaza kazi zinazofanywa na Rais Dkt Samia Suluhu Hasani ambaye ni mwanamke mwenzao.
Mjanakheri alitumia pia nafasi hiyo kuwataka kujiandaa na uchaguzi wa Serikali za mitaa mwakani pamoja na uchaguzi Mkuu 2025 kwa kujitokeza kuwania nafasi mbalimbali ili kumuunga mkono Rais Dkt Samia.
"Niwaombe wakinamama nyie ni jeshi kubwa mkiamua kumuunga mkono Rais wetu atashinda tena kwa kishindo fanyeni hivo na njia pekee ya kumuunga ni kutangaza kazi anazozifanya kwa wananchi waweze kutambua Serikali ya awamu ya sita imefanya nini hilo najua haliwashindi na pia uchaguzi wa Serikali za mitaa jitokezeni kwa wingi kugombea" alisema Mjanakheri.
Aidha Katibu huyo aliwaonya kutojihusisha na makundi kwani kufanya hivyo ni kukivuruga chama ambapo pia alitoa Elimu ya propaganda.
Mwisho
0 Comments