Header Ads Widget

TRA - LINDI YAZINDUA KAMPENI YA TUWAJIBIKE

 



Na HADIJA OMARY_LINDI...........



MAMLAKA ya mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Lindi, imezindua kampeni ya tuwajibike kwa kutoa Elimu kwa wafanyabiashara  pamoja na wanunuzi wa bidhaa wa Manispaa ya Lindi Mkoani humo lengo likiwa ni kufanya uhamasishaji wa matumizi ya mashine za kielekroniki za EFD.


Akizungumza wakati wa zoezi hilo Meneja msaidizi upande wa madeni Chacha Gotora alisema baada ya kuwatembelea baadhi ya walipakodi wa maeneo tofauti katika manispaa hiyo wengi wao wanaendelea kutumia mashine hizo za kielekroniki za EFD

 

“Changamoto ipo kwa wateja ambapo wengi wao hawana tabia ya kukagua risiti zao pindi wanaponunua bidhaa lakini pia hawapendi  risiti zao ziandikwe tini namba wala majina yao lakini tumetoa elimu na kuwasisitiza kudai risiti zenye taarifa sahihi ya manunuzi waliyoyafanya”

 


“Wenye maduka pia tumewaimiza na tumewapa Elimu na kuwaelekeza juu ya changamoto mbali mbali za utumiaji wa mashine wanazozipata endapo mashine hizo zitaalibika au wanapokosea risiti na kuelekeza utaratibu sahii wa kufuatwa ”

 

Hata hivyo Gotora alitoa wito kwa alitoa wito kwa wafanyabiashara na wananchi wa Mkoa wa Lindi na Tanzania kwa ujumla kuhakikisha wanatoa na kudai  risiti sahihi kwa kila mauzo ama manunuzi wanayoyafanya.

 

Kwa upande wake Hassan Singa mfanyabiashara wa vifaa vya ujenzi manispaa ya Lindi alisema changamoto zilizopo ambazo ni kilio cha wafanyabiashara waliowengi ni utoaji wa risiti kwa baadhi ya wafanya biashara wakubwa walipo Dar es salaam ambako wanaenda kununua bidhaa kwa ajili ya kuuza kwenye maduka yao mikoani.

 

“kunabaadhi ya wafanyabiashara waliopo Dar es salaam hasa wafanyabiashara wa Kariakoo ambako tunanunua bidhaa zetu zipo baadhi ya bidhaa tukihitaji kununua tunapewa nusu risiti hii inatufanya baadhi yetu tushindwe kununua bidhaa zao kutokana na changamoto hizo”

 


“Ombi langu kwa mamlaka husika najua kwa TRA wa Dar es salaam swala hili sio geni kwao wawafuatilie wafanyabiashara hao kwa karibu na wawachukulie hatua za kisheria” alisema Singa

 

Awali akizungumza na waandishi wa Habari ofisini kwake kabla ya kuanza rasmi kwa kampeni hiyo kaimu meneja wa TRA Mkoa wa Lindi Geoger Mapunda alisema kuwa lengo kubwa la kampeni hiyo ya tuwajibike ni kuhamasisha wafanyabisahara kulipa kodi kwa hiyari yao

 

Alisema lengo la mamlaka hiyo ni kuwafanya walipa kodi wote walipe kodi zao kwa hiyari yao bila shuruti na sio kulipa kwa adhabu hiyo ndio sababu kuwa hata vigezo vya makadilio ya kodi yanatokana na mauzo ya mfanyabiashara husika.

 



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI