Header Ads Widget

DC LINDI, MFUMO WA STAKABADHI GHARANI UMEKUWA NA TIJA KWA WAKULIMA.

 


NA HADIJA OMARY_LINDI.........


WANAUSHIRIKA wa Mkoa wa Lindi, wametakiwa kuulinda mfumo wa uuzaji wa mazao unaotumika hivi sasa wa stakabadhi gharani  kwani umekuwa na tija kwa wakulima wa korosho  na unaondoa mianya ya Rushwa

 

Wito huo umetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Lindi Shaibu Ndemanga alipokuwa anazungumza na wanaushirika  kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa huo katika Mkutano mkuu wa sita wa mwaka 2023 wa chama kikuu cha ushirika Lindi mwambao kinachojumuisha wakulima wa Halmashauri za Kilwa, Mtama na Lindi Manispaa uliofanyika katika  ukumbi wa shule ya sekondari Nyangao Halmashauri ya Mtama Mkoani Lindi

 


Ndemanga alisema kuwa mfumo huo  wa stakabadhi gharani  umeonekana kuwa ni mfumo bora Duniani katika usimamizi wa uuzaji wa mazao hivyo ni muhimu kwa wanaushirika kuulinda na kuusimamia vizuri mfumo huo.

 

Alisema ni ukweli usiopingika kwamba kabla ya kuanzishwa kwa mfumo huo wakulima walikuwa wanahangaika kutafuta masoko ya kuuza korosho zao ambapo Kilichokuja kuokoa vurugu za bei ni mfumo huo wa stakabadhi gharani.

 

“Uzuri ni kwamba mfumo huu ukisimamiwa vzuri unaondoa mianya ya Rushwa, unaondoa kabisa mianya ya watu kujipatia kipato kupitia mazao ya wakulima hivyo licha ya mfumo huo kuwasaidia wakulima lakini unamaadui, ombi langu kwenu wanaushirika twendeni  tuusimamie mfumo wa stakabadhi gharani”.

 


“kama kunamahali ambapo mnadhani panachangamoto ni afadhari tuangalie tunafanyaje kuliko kusema kama sio mfumo mzuri tuuondoe, hapa nyie wote ni mashaidi kwa namna tulivyokuwa tunazunguka na korosho zetu katika maeneo tofauti tofauti  kutafuta soko zuri. tusije tukadanganyika tukalewa na mafanikio tukataka kurudi nyuma hakuna namna yoyote unaweza kuuza mazao kiolela”. Alisisitiza Ndemanga

 

Awali akitoa taarifa ya utekelezaji wa shughuli za chama  kwa mwaka 2022/2023 mwenyekiti wa chama hiko Ismail Nalinga  alisema pamoja na mafanikio yanayopatikana kwa wakulima kutokana na mfumo huo wa stakabadhi mazao gharani lakini bado ipo changamoto ya kushuka kwa uzalishaji wa zao hilo kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa.

 


Alisema ili tija ya mfumo huo uweze kuonekana kwa wakulima ni muhimu kwa Taasisi ya utafiti wa kilimo TARI Naliendele kuendelea kutoa mafunzo ya mara kwa mara kwa wakulima ili kuendana na mabadiliko ya hali ya hewa.

 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI