Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE
Mradi wa maji uliogharimu kiasi cha shilingi milioni 12 utakaohudumia wananchi 150 katika Kijiji Cha Uliwa kata ya Iwungilo Halmashauri ya mji wa Njombe mkoani Njombe umezinduliwa na Chama Cha demokrasia na maendeleo CHADEMA kanda ya Nyasa.
Mradi huo unatajwa Kujengwa kwa nguvu za wananchi kwa kushirikiana na viongozi wa CHADEMA ambapo mmoja wa wakazi wa Kijiji hicho bwana Emmanuel Mgulo akisoma taarifa ya ujenzi wa mradi huo amesema zaidi ya wakazi 400 Wangali wanakosa maji licha ya Kujengwa kwa mradi huo.
Awali mwenyekiti wa Chadema Jimbo la Njombe mjini Regnard Danda amesema wananchi wa vitongoji vya Canada na Itowa wamekuwa wakikosa maji kwa miaka yote Jambo lililowalazimu kuchukua hatua ya kujenga mradi huo.
Rose Mayemba ni mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Njombe ambaye anasema kitendo Cha wananchi kujenga mradi wa maji kwa nguvu zao kilipaswa kufanywa na serikali ambao Ni wajibu wao kufikisha huduma muhimu kwa wananchi.
Akizungumza mara baada ya kuzindua mradi huo Mwenyekiti wa Chadema kanda ya nyasa Mchungaji Peter Msigwa amesema Kutokana na kuripotiwa kwa vitisho vya kwenda kufunga maji hayo Chadema watapambana na yeyote atakayethubutu kuzuia jitihada za wananchi katika kujiletea maendeleo.
Baadhi ya wananchi wa Uliwa akiwemo Longnus Mlowe na Agnes Nyongole Wamesema kutokana na kuchangia ujenzi wa mradi wa maji kwa muda mrefu bila mafanikio walilazimika kuanza kuchangishana wenyewe kwa kuunda Kamati yao iliyowafikisha hadi kupata maji.
Hii ni mara ya kwanza kwa chama cha upinzani kusini mwa Tanzania kushiriki zoezi la uzinduzi wa mradi wa Wananchi.
0 Comments