WATU watano wamefariki dunia kwa ajali mkoani Iringa akiwemo mwandishi wa Habari Rashid Msigwa (38) mkazi wa Igumbilo mjini Iringa na wengine wanne waliofariki dunia kwa kufukiwa na kifusi katika mgodi wa Grace Chura uliopo Kijiji cha Igomaa kata ya Sadani Wilaya ya Mufindi mkoani hapa.
Kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa Allan Bukumbi aliwaeleza wanahabari Leo ofisini kwake kuwa katika tukio la kwanza lililotokea majira ya saa 7 usiku wa kuamkia Leo April 19,2023 mwandishi wa Habari Msigwa akiwa na gari binafsi aina ya Alteza Toyota Mazda yenye namba za usajili T995 iliyokuwa ikiendeshwa na marehemu Msigwa .
Alisema kuwa ajali hiyo ilitokea eneo la Ipogolo Jirani na Stendi ya Ipogolo katika barabara kuu ya Iringa – Mbeya kuwa dereva wa gari hilo alikuwa akijaribu kumkwepa mwendesha pikipiki na hivyo kugonga pikipiki hiyo iliyokuwa ikiendeshwa Joel Mgudula (23) makazi wa Ipogolo ambae alijeruhiwa mguu.
Alisema kutokana na gari hiyo kuwa katika mwendo mkali dereva wa gari alishindwa kulimudu gari hilo na hivyo kupelekea kugonga pikipiki kisha mti na kupelekea kujeruhiwa vibaya maeneo mbali mbali ya mwili wake na wakati akikimbizwa Hospitali kwa matibabu alifariki dunia .
Kwa mujibu wa kamanda Bukumbi inasemekana Msigwa alikuwa katika mwendo mkali na ndio chanzo cha ajali hiyo hivyo kutoa wito kwa madereva kuheshimu sheria za usalama barabara na kuepuka mwendo kasi .
Kwa upande wa shuhuda wa ajali hiyo Adam Sanga ambae ni dereva boda boda eneo hilo alisema kuwa dalili za gari hilo kupata ajali walizoana hata kabla ya kumgonga mwendesha boda boda kwani gari ilikuwa ikija mbele yao kwa mwendo mkali na kjuwalazimu boda boda waliokuwepo eneo hilo la nje ya stendi la Ipogolo kukimbia kukwepa ajali ndipo alipokwenda kumgonga boda boda mwenzao aliyekuwa akijaribu kuingia stendi ya Ipogolo .
Katika tukio la pili Kamanda Bukumbi alisema kuwa zadi ya watu saba walifukiwa na kifusi katika mgodi unaomilikiwa na Grace Chura kwenye Kijiji cha Igomaa kata ya Sadani wilaya ya Mufindi ambapo jitihada za kuwatoa wahanga hao zilizaa matunda kwa watu watatu huku wanne kati yao wakipoteza Maisha .
Alisema kuwa tukio hilo limetokea majira ya saa 2.30 usiku wa kuamkia Leo April 19,2023 wakati wachimbaji hao wakiwa katika mgodi huo .
Kamanda Bukumbi alisema majira ya majeruhi na walipoteza Maisha bado kufahamika kutokana ugeni wao wa wahusika katika eneo hilo japo jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi zai ikiwa ni pamoja na kutafuta mmiliki wa mgodi huo na afisa madini ili kujua kama mgodi ulikuwa na kibali na taratibu nyingine za uchimbaji .
Alitaja chanzo cha vifo vya wachimbaji hao wadogo wa madilni kuwa ni mvua kubwa zinazoendelea kunyesha na kupelekea ardh katika mgodi huo kuwa Nyevu nyevu ( Yenye maji maji)hivyo kuporomoka.
0 Comments