Na Hamida Ramadhan Matukio Daima APP Dodoma
WAKAZI wa Jiji la Dodoma wameshtushwa na hatua inayotakwa kuchukuliwa na Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira (DUWASA) kutaka kupandisha Bei za maji kwa madai kuwa Gharama za uendeshaji na kukarabati vitendea kazi zimekuwa kubwa kwao.
Wakiongea katika kikao kilichoandaliwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji ( EWURA) mkutano uliowakutanisha wananchi wote wa jiji la Dodoma, na Wilayani lengo likiwa ni kupata maoni juu ya maombi ya DUWASA ya kutaka kurekebisha bei za huduma ya maji na usafi wa mazingira.
Akizungumza kwa niaba ya wananchi wenzake Revina Petro Lamiula Mkazi wa Mkuhungu ameitaka DUWASA kuacha kuchukua hatua ya upandushaji wa Bei ya maji na badala yake kuboresha mgao wa Utoaji wa maji jijini Dodoma.
"Pamoja na bei kupandishwa ila tunataka Mamlaka ya Maji na USafi wa Mazingira ( DUWASA) muhakikishe mnaboresha huduma zenu kwa kuboresha mgao wa utoaji wa maji kwani kunamaeneo mengine maji hayatoki kabisa na bili za maji zinarekodiwa kila mwenzi, huu ni wizi,"amesema Mkazi huyo.
Naye Emmanuel Zakaria Mkazi wa Nzuguni ameitaka DUWASA kutafakari upya wazo hilo na kutafakari upya juu ya hatua wanayotaka kuchukua ya kupandisha bei ya maji kiholela.
"Kwa hatua hii ya kupandisha bei ya maji niwazi kuwa hata Ile kampeni yetu ya kuifanya Dodoma kuwa ya kijani haitafanikiwa kwani Mwananchi hatoweza kumwagilia walau tone moja la maji katika mti wake wa matunda au wakivuli hivyo DUWASA kaeni chini mjitafakari upya ," alisema Zakaria
Aidha Wananchi hao wameiomba Mamlaka ya Maji na USafi wa Mazingira DUWASA Kuangalia ongezeko la faini kwa mtu aliyekatiwa maji kutoka 15000 hadi kufikia Shilingi Elfu 25000 na kudai kuwa huko ni kumkandamiza Mwananchi.
"Kama Shilingi 15000 Mwananchi ilikuwa inamshinda Kama faini ya kukatiwa maji nyumbani kwake Mimi naona kutupandishia faini ya Shilingi 25000 ili mtu upatiwe mita yake hiyo inamaanisha mnataka kubaki na mita za Wananchi ofisini kwenu," amesema Zakaria
Awali mwakilishi wa Mkurugezi mkuu wa EWURA Geogre Kabelwa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira DUWASA imeomba kufanya marekebisho ya bei zitakazotumika kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia mwaka 2023/24 hadi 2025/26 .
Amesema kwa mujibu wa maombi yaliyowasilishwa EWURA,Mamlaka ya Maji Dodoma imebainisha kuwa marekebisho ya bei ya maji, yanalenga kupata fedha za kutosha kukidhi gharama halisi za uendeshaji na matengenezo kwa lengo la kuboresha huduma zitolewazo.
Amesema Mamlaka ya Maji Dodoma imeeleza kuwa bei zinazopendekezwa zitaiwezesha mamlaka kumudu gharama zote za utoaji huduma pamoja na mambo mengine, kuendelea kuongeza ubora wa maji, kuiwezesha mamlaka kuwa endelevu na kukidhi matarajio ya wana Dodoma.
Naye Mkurugenzi Mtendaji DUWASA Mhandisi Aron Joseph amewata wanachi kukubali Mabadiliko ya Bei kwani mamlaka imekuwa ikikabiliwa na Changamoto ya rasilimali fedha hali inayopelekea baadhi ya mambo kutokwenda.
Kwa Upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule akiongea wakati wa ufunguzi wa kikao Cha maombi ya kurekebisha bei za huduma ya maji safi yaliyoletwa na mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira dodoma ( DUWASA) amesema lengo kubwa la Serikali katika kufanya mabadiliko haya na kuongeza uwekezaji katika sekta ya Maji.
"Serikali inataka kuongeza ubora na upatikanaji wa huduma hapa Tanzania na hivyo kuboresha maisha ya Wananchi wake na hatimaye kufikia lengo la asilimia 95 (kwa mijini) lililowekwa katika Ilani ya Chama cha Mapinduzi ifikapo mwaka 2025," amesema Senyamule.
0 Comments