Header Ads Widget

UKWEPAJI WA MAJUKUMU NDANI YA FAMILIA HUSABABISHA UKATILI WA KIJINSIA

 


Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE


Kushindwa kutekelezwa kwa majukumu ya kifamilia kwa baba na Mama yametajwa kuwa chanzo cha kuvunjika kwa ndoa na kuwasababishia madhara watoto ambao ni ukatili wa kijinsia.


Hayo yanaibuka katika semina kwa viongozi wa Chama cha mapinduzi CCM jimbo la Njombe mjini ambapo mkuu wa Dawati la jinsia mkoa wa Njombe toka jeshi la Polisi Afande Wilfred Willa anasema kila mmoja ndani ya familia anapaswa kutekeleza majukumu yake kama mila na desturi za kiafrika zinavyotutaka badala ya Baba kutaka majukumu yake kutekelezwa na mama.



Adha Afande Willa anasema Njombe bado kungali na vitendo vya ubakaji na ulawiti ambapo imefikia hatua baadhi ya wanaume wanabaka hadi mifugo.


Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Njombe Justin Nusulupila anawaomba Wanawake kusaidia katika malezi ya watoto kwani changamoto imekuwa ni kubwa katika jamii.



Baadhi ya wanachama wa CCM wameonekana kutoridhishwa na baadhi ya mambo katika familia ikiwemo kipengere cha majukumu ya baba kwenye suala la kipato huku wakisisitizwa kuwa hakuna mtu wa kuwabeba zaidi ya kuwajibika kama Baba.



Beatrice Malekela ni mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Njombe ambaye anawataka wanawake wasiwe chanzo cha kufarakanisha ndoa na kuibua ukatili katika familia.









Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI