NA HADIJA OMARY _LINDI.......
MAMLAKA ya Dawa na vifaa tiba Tanzania TMDA kanda ya kusini imewakamata watu wawili ambao majina yao yamehifadhiwa kwakujihusisha na usambazaji wa Dawa na vifaa tiba kwa kutumia pikipiki (Boda boda).
Akizungumza wakati wa zoezi hilo lililofanyika eneo la mkwajuni Halmashauri ya Mtama Mkoani Lindi barabara kuu ya Masasi jana tarehe 28 Aprili, 2023Mkaguzi wa dawa wa Mamlaka hiyo Bw. Horrace Mbungani amesema watu hao wamekamatwa kupitia zoezi la ukaguzi wa kushituza uliofanywa na mamlaka hiyo ili kubaini pikipiki zinazosambaza Dawa na vifaa tiba bila kuzingatia sheria na taratibu .
Bw. Mbungani aliesema kumekuwepo na tabia ya kusambaza dawa, vifaa tiba kwa kutumia pikipiki pasipo kuangaliwa kwa taratibu za namna bora ya kusafirishwa kwa bidhaa hizo ambapo TMDA Kanda ya Kusini imeanzisha msako maalumu kwa ajili ya kubaini watu wanaojihusisha na usambazaji huo.
" tumefanya zoezi la ukaguzi wa kushitukiza kwa pikipiki ambazo zimeonekana kuwa na matenga na kufanikiwa kukamata pikipiki mbili, lakini zingine zimekimbia baada ya kutakiwa kusimama"
"Katika piki piki hizo mbili kumebainika dawa aina mbalimbali ambazo zinatakiwa kutolewa kwa cheti katika matumizi yake, ambapo hata hivyo Wahusika tuliowakamatwa hawana taaluma wala elimu ya dawa hivyo kutofahamu namna gani kuhifadhi " alifafanua Mbungani.
Mbungani alizema kuwa zoezi hilo litakuwa endelevu na kwamba wataendelea na zoezi hilo katika maeneo yote ya kanda ya kusini.
Hata hivyo bwana Harrance alitoa rai kwa jamii kuacha kuuza dawa kwa kutumia pikipiki au vyombo ambavyo sio sahihi kusafirisha au kusambaza dawa.
0 Comments