Na Hamida Ramadhan Matukio Daima APP Dodoma
NAIBU Waziri wa Kilimo Anthony Mavunde amesema kuwa Serikali itaendeleza mazao yote nchini ikiwemo zao la Vanila na mazao ya mbogamboga,Matunda na viungo.
Mavunde amesema hayo jijini Dodoma wakati akizungumza na wadau wa zao la Vanila.
Amesema kuwa zao la Vanila lipo kwenye sehemu ya mkakati wa Serikali na leo wameanza hatua ya kwanza ya kikao Cha wadau kutekeleza njia sahihi ya kulihudumia zao hili na upatikanaji wa mazao ya uhakika.
Aidha amesema kuwa kikao hicho kitakwenda kuhakikisha zao la Vanila liwe kwenye utaratibu mzuri Kwa kutengenezewa utaratibu wa muongozo kama ambavyo wamefanya Katika mazao mengine ya mbogamboga na Matunda.
Kwa Upande Mlezi wa WAKULIMA wanaolima zao hilo la vanilla Prof.Anna Tibaijuka ameiomba serikali iwasidie kuwapatia elimu wakulima wa Vanila ili kupata taarifa sahihi za zao hilo.
Amesema licha ya kusemekana kuwa zao la vanilla nizao lenye faida kubwa kwa wanaolima lakini bado wakulima wa Vanilla wamekuwa wakipata Changamoto yakuibiwa hali inayopelekea kitoona manufaa ya kilimo chao.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa Vanilla International Limited Simon Mnkondya ameitaka jamii kutumia zao la Vanilla katika matumizi ya Kila siku kwani zao hilo huchochea kuwa na akili zilizopitiliza Kwa binadamu.
Mkurugenzi huyo amesema ili kuweza kuwa na akili nyingi,hata wanasayansi Duniani wamekuwa wakitumia malighafi inayopatika katika zao la Vanilla hali inayopelekea kuwa wabunifu na kubuni vitu mbalimbali.
Aidha Mnkondya amebainisha kuwa vyama vya ushirika vimekuwa vikiwaibia wakulima bila kuwatengenezea masoko ya uhakika na badala yake vimekuwa vikitengeneza wezi.
Pia amebainisha kuwa kilimo Cha Vanilla soko lake linapatikana Kwa wingi katika nchi za uarabuni na Vanilla inayonuniliwa sana ni Vanilla ya gradi la kwanza.
Katika kuuza zao la Vanilla Kwa Duniani ya sasa Mnkondya amebainisha kuwa haina haja ya kubeba mzigo kupeleka katika nchi unaweza kuuza kupitia mtandao Kwa kuandika vigezo vya zao lako la Vanilla na wateja wakakufata wenyewe.
Ameongeza kuwa zao la Vanilla halitakiwi kulimwa kiholela na badala yake amewashauri wakulima kulima,kulima Kwa pamoja kilimo Cha Block Farming.
Katika hatua nyingine ametahadharisha kuwa watu wanaolima zao la Vanilla wapo katika hatari ya kujiruhiwa kwani zao hilo lina bei sana na kupelekea kupata fedha nyingi.
0 Comments