BILIONI 6.06 KUONDOA ADHA YA MUDA MREFU YA WANAFUNZI KUKAA CHINI NA KUKOSA MIUNDOMBINU YENYE SIFA WAWAPO SHULENI
Serikali imeupatia Mkoa wa Rukwa shilingi Bilioni 6.06 kwaajili ya miradi katika shule 29 za Msingi, kati ya hizoi shule, 9 ni mpya.
Shule hizo 9 zimegawanywa katika sehemu mbili, shule 4 ni zile zenye mkondo mmoja na shule 5 ni zile zenye mikondo miwili, lakini pamoja na ujenzii wa shule mpya pia ukarabati kwa majengo yaliyopo utafanyika mkoani Rukwa.
Jumla ya miundombinu 176, yakiwemo madarasa 150 ya darasa la kwanza hadi la saba na madarasa 26 ya mfano kwa elimu ya awali, Matundu 237 ya vyoo, ambavyo watatumia walimu na wanafunzi wao, nyumba 2 za walimu ambazo zitakuwa zinatumika na familia mbili yaani Two in one.
Pia yatajengwa majengo 9 ya utawala katika shule za Msingi, vichomea taka 9 ili kulinda, kuhifadhi na kutunza mazingira katika shule hizo kwa sababu mpaka sasa hakuna ajuae taka zinazozalishwa shuleni zinatunzwa wapi, kama si wengine kuzifukia katika maeneo ya shule.
Kubwa Zaidi ya hayo serikali itatengeneza na kununua madawati 2,640 ya wanafunzi ambao ukienda katika shule za Msingi zilizopo wanafunzi wengi wanakaa chini. Sambamba na madawati pia serikali itatengeneza na kununua meza 26 na viti 26 kwaajili ya walimu wawapo ofisini na sehemu za kufundishia.
Serikali itanunua na kutengeneza Shubaka 26 ( cabinet za kutunzia file na mitihani ya wanafunzi), kila shule za wanafunzi wa elimu ya awali kutakuwa na bembea, pamoja na ujenzi na ukarabati wa viwanja vya michezo.
Kwa kuwa ni miradi mikubwa inayotekelezwa na serikali yenye thamani kubwa, katika kukabiliana na majanga ya moto, serikali itanunua vizima moto( Fire Extinguishers) pamoja na Vihisi Moto( fire detectors)
Hii ni kwa mujibu wa Mkuu wa Rukwa Comred Queen Sendiga ambaye ametoa taarifa hiyo kwamba hizo fedha tayari zimeletwa kwenye akaunti za Halmashauri, Halmashauri ya wilaya ya Kalambo imepokea shilingi Bilioni 1.379, Halmashauri ya wilay aya Nkasi imepokea shilingi Bilioni 1.535, Halmashauri ya wilaya ya Sumbawanga imepokea shilingi Bilioni 1.597 na Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga imepokea shilingi Bilioni 1.553.
Unahitajika usimamizi wa kina katika kutekeleza miradi hiyo ambayo inakwenda






0 Comments