NA CHAUSIKU SAID
MATUKIO DAIMAAPP MWANZA.
Chama Cha Wanasayansi wa maabara za afya (MeLSAT) kimetakiwa kuwa na maabara zenye mipango endelevu ili kukabiliana na changamoto pamoja na watalaamu wa afya katika kufanya kazi kama timu Kwa kutumia takwimu za maabara kuboresha huduma za afya katika Mkoa na Taifa Kwa ujumla.
Hayo yamebainishwa na katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza Elikana Balandya katika ufunguzi wa wiki ya wataalamu wa maabara uliyofanyika katika viwanja vya furahisha wilaya ya Ilemela Mkoani hapa.
Balandya amewataka watalaamu wa maabara kutumia maadhimisho hayo kama chachu ya kuleta mafanikio ya kiutendaji wa shughuli za maabara Kwa kuimarisha na kuboresha huduma hizo pamoja na chama kuwa na nguvu, uwezo wa kuendelea kutoa huduma Kwa wanachama na jamii Kwa ujmla
"Chama kinahitaji wanachama ambao ni wataalamu wa maabara kujiunga, hivyo natoka wito Kwa wataalamu wote wa maabara Mkoa wa Mwanza wawe wanachama hai na kushiriki katika shughuli mbalimbali za chama" Alisema Balandya.
Balandya amewataka waajiri kuwaruhusu watalamu wa maabara kushiriki katika shughuli za chama bila kuathiri shughuli za utoaji wa huduma Kwa wananchi katika Taasisi zao.
Aidha Kwa upande mwingine ameawataka waajiri wote sekta ya umma na Binafsi kutenga bajeti za kuboresha masilahi ya watalaamu na kuendeleza watumishi wa maabara.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Thomas Rutachonzibwa ameeleza kuwa huduma za maabara zimeendelea kuwa nguzo muhimu katika matibabu sahihi Kwa wagonjwa ndani ya Mkoa wa Mwanza.
"Tumeendelea kisimamia ubora wa huduma za maabara za serikali na Binafsi Kwa kufanya usimamizi shirikishi na ukaguzi" Alisema Rutachonzibwa.
Rutachonzibwa ameeleza kuwa Mkoa wa Mwanza unajumla ya maabara 314 kati ya hizo 84 ni maabara za serikali huku binafsi zikiwa ni 230 kati ya hizo 84 zimejishikiza na 146 zinajitegemea huku jumla ya wataalamu wa maabara wakiwa ni 414 na maduka ya kuuza vifaa yakiwa ni 23.
"Tumekuwa na mafanikio na mafanikio kadhaa yanayoashiria kuwa huduma za maabara zinatolewa katika ubora unaotakiwa, matharani maabara nne (4) Zina lthibati ya ubora wa huduma za kimataifa, maabara tano (5) ziko katika hatua mbalimbali za mchakato wa kupata lthibati ya kimataifa" Alisema Rutachonzibwa.
Ameeleza kuwa mbali na mafanikio waliyoyapata bado kunachangamoto mbalimbali ikiwemo na upungufu wa wataalamu wa maabara katika vituo vya kutolea huduma hasa katika vituo vipya vilivyojengwa.
Amefafanua kuwa baadhi ya maabara binafsi kutozingatia miongozo, kanuni na sheria ya kuanzishwa Kwa maabara hizo na baadhi ya wataalamu kutolipa Kwa wakati ada za kuhuisha leseni za Taaluma na kutojiunga na chama Cha kitaaluma(MeLSAT).
Kwa upande wake katibu chama Cha Wanasayansi wa maabara Mkoa wa Mwanza Yusuph Mkama amesema kuwa wanaiomba Wizara kuwa na mkakati wa kuwapangia wahitimu waliofaulu vyema katika vyuo vya sayansi za maabara za afya ili kuweza kupunguza upungufu wa rasilimali watu (Wakufunzi).
Mkama ameeleza kuwa kumekuwa na utaratibu wa baadhi ya wamiliki wa maabara kuajili wataalamu wasio na sifa na kuwaacha wataalamu wenye sifa Kwa kisingizio Cha kupunguza gharama.
" Hii inaathiri afya za wananchi na kuongezea gharama za matibabu kwani majibu yananyotolewa yanakuwa hayana ubora na pengine hayana ukweli ndani yake, pia tatizo Hilo limeathiri taswila ya taaluma yetu na kuonekana haifanyi katika kufanya uchunguzi wa magonjwa na kupunguza uaminifu Kwa wagonjwa" Alisema
Katibu Mkuu wa Taifa wa Chama cha Wanasayansi wa Maabara za Afya Tanzania (MeLSAT)Betrad Msemwa amelipongeza Serikali kwa kujenga vituo vya afya na kupelekea vifaa tiba kila sehemu kwani imepelekea wananchi kupata huduma kwa wakati.
Hata hivyo ameiomba Serikali kuendelea kuajiri wataalam wa maabara ili waweze kufanya kazi katika kiwango kinachotakiwa kwa kutoa huduma kwa wananchi Kwa wakati











0 Comments