NA CHAUSIKU SAID_MATUKIO DAIMAAPP MWANZA
Mwanamke mmoja ajulikanae Kwa jina la Sara Robert mwenye umri wa miaka (33) Mkazi wa Nyashitale Wilaya ya Sengerema Mkoani Mwanza anatuhumiwa kuiba Mtoto wa kiume mwenye umri wa miezi mitatu(3).
Kamanda wa polisi Mkoani hapa Wilbroad Mtafungwa akitoa taarifa hiyo mbele ya waandishi wa Habari ameeleza kuwa chanzo Cha tukio Hilo ni mume wa Sara kuhitaji kupata Mtoto wa kiume .
Mtafungwa ameeleza kuwa Mtuhumiwa alikiri kuhusika na wizi wa Mtoto huyo na kudai kuwa alifanya hivyo kutaka kumridhisha mume wake Kwa kumhadaa kuwa amepata Mtoto wa kiume kutokana na yeye kubahatika kupata watoto wa kike peke yake.
"Alitamani kuona na yeye anapata Mtoto wa kiume ndipo akaishia kufanya wizi na hatimaye akakamatwa na utaratibu wa kumfikisha mahakamani inafanyika haraka ili aweze kujibu mashtaka yake" Alisema Mtafungwa.
Aidha ameeleza kuwa kutokana na uchunguzi kuendelea kufanyika Mtoto amewwza kukabidhiwa Kwa wazazi wake ili kuendelea na malezi.
0 Comments