Header Ads Widget

WANAWAKE TANESCO NJOMBE WAPANDA MITI



Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE


Ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi yanayolikabili taifa kutokana na uharibifu wa vyanzo vya maji na kusababisha mito kukauka na kukwamisha jitihada za upatikanaji wa nishati ya umeme wa uhakika wakati wote,Wafanyakazi wanawake wa shirika la umeme Tanzania Tanesco mkoa wa Njombe wameamua kwenda kupanda miti aina ya mivengi katika Chanzo cha maji cha Howadi kibena kuelekea katika kilele cha siku ya wanawake duniani.



Zoezi hilo limefanyika baada ya shirika la umeme TANESCO Mkoa wa Njombe kununua miti hiyo ambayo imekuwa mworobaini wa utunzaji mazingira na vyanzo vya maji ambapo Meneja wa shirika hilo mkoa wa Njombe Mhandisi Andrew Lucas amesema hii itasaidia kupunguza changamoto ya kukatika kwa umeme mara kwa mara.


Aidha Afisa rasilimali watu Tanesco mkoa wa Njombe Frida Barankena anasema maadhimisho ya siku ya wanawake ambayo hufanyika kila machi nane ya mwaka yamewasukuma kuona umuhimu wa kuboresha mazingira kwa kupanda miti hiyo kwenye vyanzo vya maji.



Hata hivyo Afisa uhusiano kwa wateja Tanesco mkoa wa Njombe Lucy Mtani anasema hii ni moja ya shughuli za kuunga mkono jitihada za serikali za kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.



Wakazi wa Kibena wakiongozwa na afisa mtendaji wa mtaa wa Kibena Hospitali Izack Ng'ande na Romanus Mlowe ambaye ni muwatikaji wa miche ya aina mbalimbali ikiwemo ya uhifadhi ya mazingira wanapongeza jitihada za Wanawake wa Tanesco kufika katika eneo hilo kupanda miti na kwamba kinachotakiwa jamii inapaswa kuwaunga mkono kwa kutunza mazingira.



Tanesco wenyewe wanasema''PANDA MITI,MVUA NDI,UMEME NDINDINDI"

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI