Header Ads Widget

USAWA WA KIJINSIA KUTOKOMEZA UKATILI KWA WANAWAKE.

 


MKUU wa Wilaya ya Kibaha Nickson John amesema kuwa usawa wa kijinsia ni kutokomeza ukatili na ubaguzi dhidi ya wanawake na wasichana na kuhakikisha wanapata fursa za sawa katika umiliki rasilimali.


John ameyasema hayo Mjini Kibaha wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani kwenye Halmashauri ya Mji Kibaha ambapo aliwakilishwa na katibu Tawala wa Wilaya ya Kibaha Sozi Ngate.


Amesema kuwa ili kufanikisha lengo hilo ifikapo 2030 serikali imetekeleza mikakati mbalimbali ya kuondoa aina zote za ukatili na ubaguzi dhidi ya wanawake na wasichana kwa kutambua matendo hatarishi na ukatili na kutoa huduma stahiki kwa walioathiriwa na matendo hayo.


"Kutoa fursa katika kuwania nafasi za uongozi, umiliki wa ardhi, kujumuisha masuala ya kijinsia katika shughuli za serikali za mitaa ili kukabiliana na vikwazo,"amesema John.                


Kwa upande wake ofisa maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya Mji Kibaha Leah Lwanji amesema kuwa kipindi cha mwaka 2021/2022 wajasiriamali kwa makundi ya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu walikopeshwa mikopo yenye thamani ya shilingi milioni 894.8kwa vikundi 158. 


Naye mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kibaha Mhandisi Mshamu Munde amesema kuwa fedha hizo siyo kwa ajili ya kugawana bali ni za kuzalisha ili watu wengine nao waweze kukopa. 


Wakihamasisha uhifadhi wa Mazingira kwenye sherehe hizo Shirika la Scientific Agri-Forest and Humanity Organization (SAHO) kupitia mkurugenzi wake Emanuel Luhamba amesema kuwa wamepanda miti 90 kwenye barabara za kuelekea Halmashauri ya Mji Kibaha.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI