NA HADIJA OMARY,MATUKIO DAIMAAPP
LINDI
…….mradi wa Mwananchi wajibika kufuatilia matumizi ya rasilimali za umma kwenye sekta ya Afya Unaotekelezwa na Shirika la usaidizi wa kisheria mingoyo (SHIMKIMI) umekutana na changamoto za usiri wa upatikanaji wa taarifa kutoka kwa watendaji wa Zahanati na Vituo vya Afya Manispaa ya Lindi Mkoani humo.
Hayo yamebainishwa na Mratibu wa Mradi huo wa Mwananchi wajibika kufuatilia matumizi ya rasilimali za umma kwenye sekta ya Afya unaofanywa na Shirika hilo la usaidizi wa kisheria Mingoyo (SHIMKIMI) kwa ufadhiri wa shirika la foundation for civil society (FCS) Bw.Kasimu Mapande katika kikao cha kuleta mrejesho wa mradi huo.
Mapande alisema Licha ya kufanya kazi hiyo ya ufuatiliaji kwa kupata kibali kutoka ofisi ya Rais TAMISEMI pamoja na barua kutoka kwa mkurugenzi wa Manispaa hiyo lakini wapo baadhi ya viongozi wa vituo vya Afya na Zahanati walizohitaji kufanya nazo kazi waligoma kutoa taarifa za vituo vyao.
Alisema mradi huo ulikuwa unafanya ufuatilia miradi ya ujenzi wa Zahanati na vituo vya Afya ambapo kwa kiasi kikubwa changamoto hiyo ilipunguza ufanisi wa utendaji kazi kwenye ufuatiliaji na wa mradi huo
Alisema hali hiyo inaweza ikawa inachochewa na kasumba ambayo imezoeleka kwa muda mrefu ya kuwepo na usiri katika uendeshaji wa miradi mbalimbali ya Umma na binafsi.
Nae mkurugenzi wa shirika hilo la usaidizi wa kisheria Mingoyo (SHIMKIMI) Nuhu Mkapanda alisema lengo kubwa la kufuatilia miradi hiyo ilikuwa ni kuongeza uwajibikaji kwa jamii ili kuongeza ubora wa bidhaa na huduma kwenye sekta ya Afya kwenye kata tatu za manispaa ya Lindi ambazo ni Mingoyo, ng’apa na Chikonji.
Alisema lengo linguine lilikuwa ni kuimarisha uwezo wa uwajibikaji, uwazi na ushirikishwaji wa wananchi na wadau wa Afya katika utekelezwaji wa miradi mbali mbali ya maendeleo kwenye Sekta ya Afya katika halmashauri ya manispaa ya Lindi.
Akifunga kikao hiko mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Afisa tarafa ofisi ya mkuu wa Wilaya Heriet kaluwa alisema swala la watumishi wa umma kuficha taarifa kwa mtu ama taasisi zilizopo kisheria ni kinyume na taratibu za kiutumishi
Aliwataka watumishi hao kuacha mara moja Kuficha taarifa zinazoombwa kisheria kwa mtu ama taasisi za kiserikali na zisizo za kiserikali kwa lengo la kuweka uwazi na uwajibikaji
0 Comments