Header Ads Widget

SERIKALI KUBORESHA MIUNDOMBINU YA MAWASILIANO MIPAKANI

 


Teddy Kilanga,Arusha


Serikali ipo kwenye mkakati wa uboreshaji wa huduma za mawasilino katika maeneo mbalimbali nchini ikiwemo mipakani ili kuondokana na changamoto ya mwingiliano wa mitandao na nchi jirani ya Tanzania.


Waziri wa habari ,mawasiliano na Teknolojia ya Habari,Nape Nnauye amebainisha hayo katika uzinduzi wa mnara wa mawasiliano ya simu katika kata ya Noondoto wilayani Longido mkoani Arusha.


"Kule ambapo minara haipo kabisa tutaongeza na hasa maeneo ya mipakani kwani nimechoka kusikia wananchi wetu wanatumia mitandao ya nchi jirani hivyo sasa hivi tunataka tuongeze nguvu ili majirani zetu pia watumie,"alisema Waziri.


Nape alisema katika hilo serikali itahakikisha inamuunganisha kila mtanzania na huduma ya mawasiliano ili waweze kujiinua kiuchumi na kuleta maendeleo nchini.


"Tutajitahidi kadri inavyowezeka huduma ya mawasiliano inawafikia wananchi hasa katika maeneo ya vijijini kwani serikali inatenga fedha kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya mawasiliano,"alisema Waziri Nnauye.


Hata hivyo aliwataka wananchi kutumia huduma hizo kwa matumizi chanya ya kuleta maendeleo ili kujiepusha na mkono wa sheria endapo wakitumia vibaya tofauti na matarajio ya uwekezaji huo.




Mtendaji mkuu wa mfuko wa mawasiliano kwa wote(UCSAF) Justina Mashiba alisema katika mkoa wa Arusha wametekeleza miradi 36 ikiwa 27 imeshakamilika ambapo mnara huo wa tigo wamechangia takribani sh.104.9 kwa ajili ya ukamilishaji wa ujenzi wa mnara huo.


"Sehemu kubwa iliyokuwa na changamoto ya mawasiliano ni kata ya Noondoto lakini baada ya kuwashwa mnara huu umeweza kuwafikia wananchi wa Monduli, lakini katika kata ya Longido inajumla ya miradi 11 ambayo inaendelea kutekelezwa,"alisema 


Meneja wa mauzo wa kampuni ya simu tigo ,Oliver Baltazary alisema mradi huo umegharimu zaidi ya  sh.milioni 250 ambapo asilimia 40.9 ya fedha hizo zimetoka UCSAF ambapo mkataba ulisainiwa  April 27,2022  na kukamilika julai Mwaka huo huo.



"Mnara huo unauwezo wa 3G na 2G ambayo inawezesha mawasiliano ya kutumia mtandao,"alisema Baltazary.


Baadhi ya wakazi wa Kata hiyo wamesema wanaishukuru serikali kwa kushirikiana na kampuni ya tigo kwa kuwasogezwa huduma ya mawasiliano kwani hapo awali walikabiliwa na changamoto ya kutembea umbali mrefu takribani kilometa 10 kufuata huduma ya mawasiliano.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI