Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Adam Malima amefungua Mafunzo ya Ushauri Nasihi yaliyofanyika katika Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kilichopo eneo la Mkolani Jijni Mwanza na yaliyowakutanisha watendaji mbalimbali ishirini na sita kutoka ndani ya mikoa ya Tanzania
Akizungumza kwenye mafunzo hayo RC Malima amewataka washiriki wa mafunzo ya Dawati la Jinsia na Ushauri Nasihi kuhakikisha wanaelewa mada zinatoloewa za Unyanyasaji wa kijinsiai ili kuhakikisha wanakwenda kuitokomeza kwa jamii.
Aidha Mhe Malima ametoa wito kwa menejimenti za Vyuo Vikuu na Taasisi za Elimu ya juu Nchini ambazo bado hawajaanzisha madawati hayo ya kutoa mafunzo ya Ushauri Nasihi nazo ziwezi kuanzisha madawati hayo.
Naye Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania teknolojia za kujifunzia na huduma za mikoa, Profesa Alex Makulilo amesema wamekuwa na utaratibu wa kutoa mafunzo hayo ya kuwajengea uwezo wa kumudu changamoto mbalimbali sababu wafanyakazi wengine kwenda kufanya kazi katika taasisi zingine pia wengine huwa ni waajiriwa wapya ambao hawajajengewa uwezo.
Makamu Mkuu wa Chuo hicho Profesa Elias Bisanda amesema chuo hicho kitaendelea kushirikiana na Jeshi la Magereza kwa kuwapa elimu wafungwa wenye nia ya kujiendeleza ili nao waweze kutimiza ndoto zao wakiwa gerezani.
0 Comments