Header Ads Widget

SERIKALI YAWAAGIZA WAKURUGENZI WA HALMASHAURI KUWAPATIA MAFUNZO YA FCC WAZALISHAJI BIDHAA

 


Teddy Kilanga Arusha.


Serikali mkoani Arusha imewaagiza wakurugenzi wa halmashauri wa mkoa huo kubaini vikundi yanayojihusisha na uzalishaji wa bidhaa zao ili kupata mafunzo kutoka Tume ya Ushindani (FCC) kwa lengo la kuongeza tija katika  mnyororo wa thamani kwenye nyanja za kibiashara.


Katibu tawala wa mkoa wa Arusha,Misaile Musa ametoa agizo hilo wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya uhamasishaji wa masuala ya ushindani na Udhibiti wa Bidhaa Bandia kwa wazalishaji Kanda ya Kaskazini yaliyofanyikia Jijini Arusha.


"Wakurugenzi wa halmashauri hakikisheni makundi haya yanapata semina za namna hii ili kuongeza tija na mnyororo wa thamani katika utekelezaji wa shughuli zao na suala hili litafanikiwa  kwa kujenga ushirikiano wa kiutendaji na Taasisi hizo za serikali,"alisema .


Hata hivyo aliipongeza FCC kwa kuendelea kutoa elimu kwa wadau mbalombali wa maendeleo na umma kwa ujumla pamoja nakufanya vizuri katika nyanja ya udhibiti wa bidhaa bandia nchini kwa kufanya kaguzi katika maeneo ya wafanyabiashara na wazalishaji wa bidhaa.


"Hivyo basi  Wakurugenzi wote wa mamlaka za serikali za mitaa katika mkoa wa Arusha hakikisheni mnakuwa na mpango kazi mzuri utakaosaidia kuratibu mafunzo ya namna hii kwa ajili ya makundi yote yanayonufaika na mikopo au fedha za serikali zinawagusa wanawakw,vijana na wenyeulemavu,"alisema Katinu Tawala huyo.


Pia alisema mafunzo hayo yatakuwa chachu ya kuogeza weledi katika nyanja za uzalishaji,uuzaji,ununuzi na utambuzi wa bidhaa bandia ikiwa ni pamoja na kujua misingi bora ya ushindani wa soko  na uchumi kwa ujumla.


Naye Mkuu wa FCC Kanda ya Kaskazini,Nonge Juma alisema mafunzo hayo kwa wafanyabiashara wa viwanda vidogo vya kati na vikubwa yanalengo la kuwezesha kuleta tija katika ushindani wa biashara wanazozalisha ikiwemo kudhibiti bidhaa bandia  zisizizosajiliwa na kuleta athari kiuchumi.


Alisisitiza wafanyabiashara hao na wenye viwanda kuhakikisha wanazongatia maadili ya biashara ili kuhakikisha soko linabaki shindani .


Huku Mwenyekiti wa Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI),Anup Modha alitoa rai kwa wamiliki wa viwanda,wafanyabiashara mbalimbali kuzalisha bidhaa zenye ubora na kuleta ushindani katika masoko kwa kuzingatia ushindani wa masoko wa ndani na nje ya nchi.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI