WATU wasiojulikana wamemuua kwa kumchinja kichwa na Kuondoka na mkono ,mguu poja na kichwa Cha mwanamke mkazi wa Kijiji cha Ilambilole wilaya ya Iringa mkoani hapa Anitha Titus Mbilinyi (48) na mwanae Andrea Mbwilo (7). Akizungumza na Matukio DaimaTv shuhuda wa tukio hilo walisema kuwa tukio hilo lilitokea Februari 10 majira ya jioni katika mpaka wa Kijiji cha Ilambilole na Matembo wakati mwanamke huyo na mtoto wake wakitoka shamba kufanya kazi za kibarua cha kupalia mahindi. Elitha Belo ambae ni rafiki wa marehemu huyo alisema kuwa kabla ya taarifa ya kifo chake alipata kukutana na marehemu na kuzungumza nae na kumwahidi kumlipa deni lake la shilingi 2000 alilokuwa akimdai. “ Nilikutana na marehemu Anitha siku mbili kabla ya kifo chake na aliniomba radhi kwa kuchelewa kunilipa deni langu la shilingi 2000 na alisema kuwa jumapili nitakuwa nimepata fedha nitakulipa nikamwabia hakuna shaka ila nimesikitishwa kupokea taarifa ya kifo chake cha kinyama” alisema Elitha Kuwa siku ya Ijumaa jioni ndipo waliposikia ngoma ya Kijiji ikipigwa kujulisha hali wananchi hali isiyo ya kawaida iliyotokea kijijini hapo . Alisema baada ya kufika ofisi ya Kijiji ndipo walipoelezwa juu ya kutokea kwa tukio la mauaji ya mwanamke huyo na mwili wake kutelekezwa kando la barabara ya lami kijijini hapo umbali wa Kilomita kama moja hivi kufika eneo la shule ya Sekondari Ilambilole. Alisema baada ya kufika eneo hilo waliukuta mwili huo ukiwa hauna kichwa ,mguu mmoja na mkono mmoja baada ya watu hao waliotekeleza unyama huo kuondoka na viungo hivyo . Jane Titus Mbilinyi Mdogo wa marehemu Akizungumza kwa niaba ya ndugu wa marehemu huyo mdogo wa marehemu Jane Titusi Mbilinyi alisema kuwa dadake alikutwa na umauti majira ya saa 12 jioni wakati akielejea kutoka shambani akiwa na mtoto wake Andrea Emannuel Mwilo aliyekuwa akisoma darasa la pili shule ya msingi Ilambilole Alisema kuwa wauaji hao walipotekeleza mauaji hayo walitoweka na baiskeli ambayo alikuwa ameazima kwa rafiki yake aliyemtaja kwa jina mmoja (jina limehifadhiwa)ambaye hadi leo rafiki yake huyo hajulikani alipo . Hata hivyo alisema kabla ya kifo kumkuta alipata kuwasiliana nae kwa njia ya simu na akimsisitiza hali ya Maisha ni ngumu na kumtaka mdogo wake huyo kuendelea kupambana na maisha . “ Dadangu baada ya kuwasiliana kwa njia ya simu alinisisitiza kuwa tuendelee kupambana na Maisha ili kulea familia nay eye aliniambia kuwa amepata kazi ya kupalilia mahindi shambani “ Alisema kuwa mtoto Andrea yeye alimfuata mama yake shambani baada ya kurejea kutoka shule majira ya saa 5 asubuhi ndipo kifo kilipomkuta huko. Alisema kuwa marehemu alikuwa na Watoto watano akiwemo Andrea aliyefariki na kati ya Watoto hao Watoto watatu wa baba mmoja na Watoto waliobaki kila mmoja na baba yake na kuwa baba wa Watoto wote walishafariki. Mwenyekiti wa serikali ya kitongoji cha Kihesa Kijiji cha Ilambilole Angela Nyalusi alisema kuwa taarifa ya mauaji hayo baada ya kuipata walitangaziana kila mwenyekiti wa kitongoji kufanya upelelezi wa kutambua watu wanaolimia mashamba yao eneo la Matembo kutokana na mwili wa mwanamke huyo kutojulikana kwa kuwa kichwa na nguo walitoweka nazo wauaji hao . “ Baada ya kutangaziana wenyeviti wote ndipo ilipobainika kuwa Anitha Mbwilo aliondoka nyumbani toka Ijumaa Kwenda eneo hilo la Matembo na hakurejea ijumaa hiyo hadi usiku” Alisema wakati wakitafuta kichwa na viongo walivyotoweka navyo wauaji hao porini ndipo walipozikuta nguo za marehemu na wakati wakitafuta zaidi walikuta kichwa kikiwa kimetupwa kwenye shimo la mchwa na walipokitoa walikuta na kichwa cha mtoto wake na viungo vingine mguu na mkono japo hadi sasa kitovu cha marehemu bado hawajakiona maana waujaji hao walikata chini ya tumbo na kuondoka na kitovu chake . Mwenyekiti huyo alisema kwenye eneo lake hakuwahi kupata taarifa zozote mbaya juu ya marehemu huyo wala hakuna matukio yoyote ya ugomvi yaliyopata kutokea yakimhusisha marehemu huyo. Huku mwenyekiti wa serikali ya Kijiji cha Ilambilole Jeiros Kiuno alisema kuwa tukio hilo ni la kwanza kutokea katika Kijiji hicho na kuwa hadi sasa Kijiji kinaendelea na msako wa kuwasaka wahusika na mauwaji hayo . “ Mimi taarifa ya mauaji haya nilipata kutoka kwa mwanakijiji mwenzetu aliyekuwa akitoka shamba japo wakati huo wa siku ya ijumaa ilikuwa ni usiku ndipo tulikubaliana utafutaji wa viungo uanze jumamosi na tulifanikiwa kukuta viungo na mwili wa mtoto wake” Alisema mwili wa mwanamke huyo na mwanae alichukuliwa na jeshi la polisi kwa uchunguzi zaidi na wanatarajia kuzikwa leo Kijiji cha Ilambilole . Kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa kamishna msaidizi wa polisi (ACP) Allan Bukumbi alipotafuta kwa njia ya simu ili kuthibitisha tukio hilo hakupatikana . Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Iringa ambae ni mkuu wa wilaya ya Iringa Veronica Kessy alipotafutwa kwa njia ya simu alisema kuwa yupo safarini mkoani Mwanza na kumtaka mwandishi wa Habari hizi kuwasiliana na katibu tawala wa wilaya ya Iringa . Kwa upande wake katibu tawala wa wilaya ya Iringa Stomen Kyando alithibitisha kutokea kwa maujaji hayo na kuwa taarifa alizopata ni kuwa hadi sasa watu wawili wanashikiliwa na jeshi la polisi kwa uchunguzi zaidi . Mganga mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Iringa Dkt Alfred Mwakalebela alithibitisha kupokea miili ya marehemu hao.
Marehemu Anitha Titusi Mbilinyi enzi wa uhai wake
Mtoto Andrea Mbwilo enzi za uhai wake
Eneo ambalo mauaji yalitokea
Shuhuda wa tukio
Waombolezaji msibani
Kijiji Cha Ilambilole
Post a Comment
0
Comments
MAGAZETI
NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI
TV News
World News
UZA NUNUA NASI LEO
Subscribe Us
MATANGAZO
TIBA YA UKANDAJI WA MGONGO, KICHWA KUTOKA NEEMA BEAUTY, SPA SALOON
0 Comments