Header Ads Widget

JUMUIYA YA WASIOONA TANZANIA WAIOMBA SERIKALI KUWAPA KIPAUMBELE HUDUMA YA BIMA YA AFYA.

 


NA CHAUSIKU SAID_MATUKIO DAIMAAPP MWANZA.


Jumuiya ya wasioona Tanzania wameiomba serikali kuwapa kipaumbele katika huduma ya bima ya afya watoto wasioona kutokana na wazazi wao kutokuwa na uwezo na wengine kutoona umuhimu wao kutokana na ulemavu walionao.


Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Omary Itambu katika Kongamano la kujadili changamoto wanazowakabili na namna ya kuzitatua katika kuelekea maadhimisho ya kumbukizi ya mwanzilishi wa maandishi ya wasioona yatakayofanyika Jijini Mwanza.


Itambu ameeleza kuwa wazazi wengi bado wanawachukilia watoto wenye ulemavu hususani wasioona kama ni mkosi katika familia hali inayopelekea kutowapa kipaumbele katika maswala ya afya na kuona kama wanapoteza fedha zao.



"Kukosekana uelewa na elimu katika jamii juu ya watu wasioona kuna pelekea kutoona uthamani wao katika jamii na kutowapa kipaumbele katika maswala mazima ya afya na kushindwa kuwa hudumia" Alisema Itambu.


Amesema kuwa ili Mtoto aende shule lazima awe na afya njema, na mtu mwenye ulemavu anaweza kusoma na anauwezo wa kufanya chochote ambacho mtu asiye na ulemavu anaweza kuifanya.


Kwa upande mwingine ameeleza kuwa mbali na changamoto walizonazo serikali imejitahidi kuwatengea fedha Ili kuhakikisha wanapata elimu iliyo Bora bila matatizo yeyote Yale.


Itamba ameiyomba serikali kuangalia mtaala wa elimu maalumu kusambazwa katika vyuo vikuu na liwe somo la lazima Kwa wanachuo wote ili kupata wataalamu na  wanapohitaji wataalamu hao wawepo na itasaidia kupata wataalamu wa kutosha.



Ameeleza kuwa serikali kuendelea kutambua michango ya waalimu wa elimu maalumu ambao wako katika tasnia ufundishaji ili kujiona serikali imewapa kipaumbele ili waweze kuhamasisha wengine kupenda masoma Hayo maalumu na kufanya kazi Kwa wito.


" Nafikiri ukitoka uhamasishaji Kila mtu atapenda kazi yake na atafanya kw ueledi kutokana na uhamasishaji unaondelea" Alisema Itambu.


Mgeni rasmi katika kongamano Hilo Greyson Lazaro Mwakilishi wa Mkurugenzi wa elimu maalumu kutoka Wizara ya elimu sayansi na Teknolojia ameeleza kuwa kumekuwa na changamoto mbalimbali zinazowakabili ikiwemo upungufu wa vifaa vya kujifunzia na mtazamo hasi katika jamii na wazazi juu ya watoto wasioona.



Lazaro ameeleza kuwa tangu mwaka 1950 elimu maalumu ilipoanza kutolewa serikali imezidi kuweka mazingira rafiki ya kupata elimu na zaidi ya shule 165 za Msingi zimejengwa Nchi nzima ili kuweza kupata elimu iliyo Bora.


Ameitaka jamii na mashirika kuendelea kushirikiana na serikali kuwafichua watoto wenye ulemavu wanaofichwa ndani kutolewa ili waweze kupata haki yao.


Kwa upande wake mwakilishi kutoka chuo kikuu Dar_ es salaam Mashukura Habibu amabye pia ni mwalimu wa elimu maalumu Bukoba ameeleza kuwa watu wenye mahitaji maalumu elimu yao ni gharama kote duniani hivyo na kuwataka wadau kuendelea kuwekeza nguvu kwani swala Hilo haliepukiki.



" Tukiweka nguvu hakuna mtu mwenye mahitaji maalumu atayeishia darasa la Saba kama Zamani " Alisema Habibu.


Habibu ameiyomba serikali kuendelea kumwezesha vifaa katika maktaba ili kuwe na elimu jumuishi ili mtu mwenye ulemavu aweze kujisomea mwenyewe bila kumtegemea mtu mwingine.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI