Na WAF- DOM
NAIBU Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel ameweka wazi kuwa, Bima ya Afya kwa wote ndio suluhu ya changamoto za magonjwa yote, kwani wananchi watatibiwa magonjwa yote ikiwemo ugonjwa wa Selimundu bila gharama kuanzia ngazi ya zahanati hadi hospitali ya taifa.
Dkt. Mollel amesema hayo leo Februari 10, 2023 wakati akijibu swali la nyongeza la Mhe. Joseph George Kakunda katika Mkutano wa kumi kikao cha tisa, Bungeni Jijini Dodoma.
Amesema, licha ya Wizara ya Afya kuendelea kuhamasisha wananchi kujiunga katika mfuko wa bima ya afya, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia Serikali yake ya awamu ya sita ameendelea kutoa fedha kwaajili ya ununuzi wa vifaa vya matibabu ya magonjwa hayo.
Ameendelea kusema kuwa, ameendelea kusema kuwa, tayari Bilion 11.5 zimetolewa na Mhe. Rais Dkt. Samia kupitia Serikali yake kwaajili ya ununuzi wa kifaa chenye uwezo wa kupima vinasaba ili kutambua tatizo hilo na kulitibu.
Aidha, Dkt. Mollel amesema, tayari Hospitali za Rufaa za Mikoa zimeanza kutenga 10% ya mapato yake ya bima kwaajili ya kuwasaidia wagonjwa wa seli mundu ili waweze kupata matibabu.
Mwisho.
0 Comments