Header Ads Widget

MKANDARASI WA REA ADAIWA KUKWAMISHA MIRADI YA REA

 


Teddy Kilanga_Arusha


Mkandarasi wa nishati vijijini(REA) aliyejulika kwa jina la Siao Ndushuka adaiwa kukwamisha juhudi za serikali kwa kushindwa kufikisha huduma hiyo katika vijiji 43 kati ya 44 katika halmashauri ya Arusha,Meru na Ngorongoro.


Miradi hiyo ya REA ilianza kutekelezwa Machi 2022 ambapo unatarajiwa kukamilika juni,23 mwaka huu nakutarajiwa kuanza kwa awamu nyingine februari 6,2023.


Akizungumza katika kikao cha utoaji wa taarifa ya utekelezaji miradi ya REA awamu ya tatu mzunguko wa pili unaolenga kufikisha umeme  katika vijiji 103 vilivyopo  mkoani Arusha,Mjumbe wa bodi ya wakurugenzi wa nishati hiyo,Styden Rwebangila amesema serikali imetoa kipaumbele cha umeme ili kuongeza chachu ya maendeleo.



"Tunaamini katika upatikanaji wa nishati ya umeme unasaidia vitu vingi na katika hili tutakuwa  tumesaidia katika afya,elimu na mambo mbalimbali ya kiuchumi,"amesema Rwebangila.


Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Arusha ambaye ni Mwenyekiti wa kikao hicho amesema katika mradi huo serikali imetoa takribani bilioni 44.4 kwa ajili ya ukamilishaji wa nishati hiyo.


"Tunachokitegemea REA kwa kushirikiana na mkoa tuwasimamie wakandarasi hawa wakamilishe miradi hii kwa wakati ili tuweze kupata thamani halisi ya fedha iliyowekezwa,"amesema Mongella.


Kwa upande wake Mkandarasi anayetekeleza mradi katika maeneo hayo,Muhandisi Siao Ndashuka amekiri na kuhaidi serikali mkoani Arusha ifikiapo juni 23 mwaka huu vijiji vilivyobaki vitakuwa vimeshapata umeme.


"Lakini mkataba wetu wigo wake mkubwa umejikita katika wilaya ya Ngorongoro ambapo tulikutana na changamoto ya eneo la hifadhi ya wanyamapori ngorongoro kutokana na serikali kusitisha huduma katika vijiji vilivyomo katika hifadhi hiyo hivyo ilibidi tutafute vijiji vingine,"alisema.


Huku Muhandisi Shuda Nyanzi anayeshughulikia na halmashauri ya Karatu,Monduli na Longido ameeleza kuwa wameshakamilisha vijiji 34 ambapo 30 wameshawasha nishati ya umeme ikiwa vinne vimebaki katika hatua za kaguzi ili kukamilisha ikiwa vijiji 17 vipo katika hatua ya ujenzi.


Naye mmoja wa washiriki wa kikao hicho ambaye ni mwakilishi wa Mbunge wa Arumeru Mashariki,Creino Issangya amesema mkandarasi huyo amekuwa sehemu ya kukwamisha miradi ya maendeleo kutokana na kushindwa kufanya kazi kwa wakati hali ambayo inawakatisha tamaa wananchi wenyw uhitaji wa huduma ya nishati ya umeme.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI