WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni amelitaka Shirika la Uzalishaji Mali la Magereza (SHIMA) kuhakikisha inatumia Ardhi ya Gereza la Isupilo wilayani Mufindi mkoani Iringa kuongeza kasi ya uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara .
Akizungumza jana baada ya ziara yake katika gereza la Isupilo waziri Mhandisi Masauni alisema kuwa mbali ya kuanza kazi kwa SHIMA ila amefarijika na mapokeo makubwa ya mabadiliko ndani ya jeshi la magereza hasa katika mkoa wa Iringa kutokana na jinsi walivyopokea mabadiliko hayo mapya .
Hivyo alisema uwepo wa SHIMA ni fursa kubwa kwa magereza kutimiza majukumu yao pia kunufaika zaidi ya shirika hilo kiuchumi kama gereza na wafungwa wanaomaliza muda wao .
Alisema kuwa jambo kubwa shirika ni kusimamia shughuli za kibiashara zitakazotokana na kilimo huku magereza wao watafanya shughuli za kusimamia wafungwa kwa kuripoti wa kamishana wa magereza Tanzania huo shirika msimamizi wake atakuwa mkurugenzi mkuu wa shirika .
Hivyo alisema makubaliano kati ya shirika na jeshi la magereza kwa wafungwa yatakuwa ya kibiashara kati ya pande hizo mbili na itasaidi magereza na wafungwa kupata faida ya nguvu wanazotumia .
" Sioni ubaya wowote kwa jeshi la magereza kuwalipa wafungwa watakaomaliza vifungo vyao kwa nguvu watakayoitumia "
Novemba 3, 2022, ndipo waziri Mhandisi Masauni alipozindua Bodi SHIMA ikiwa ni maono ya kibiashara na utekelezaji wa azma ya Rais DKt Samia Suluhu Hassan ambapo moja ya kipaumbele chake ni kuboresha Jeshi na mifumo yake.
Masauni alisema katika kutekeleza mipango hiyo, Rais aliongeza Bajeti ya jeshi hilo, ili kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao ipasavyo kwa ufanisi na weledi.
Alisema kutoka na wajumbe wa bodi hiyo aliowateua kwa sifa na weledi wao, serikali ina matumaini makubwa kuwa watatekeleza majukumu yao kwa uzalendo wa kusaidia Taifa katika Jeshi la Magereza kusonga mbele zaidi.
"Ndugu wajumbe, lengo kuu la SHIMA ni kusaidia Jeshi la Magereza kutenganisha majukumu ya kijeshi na biashara bila muingiliano wowote, ili kuwepo kwa mafanikio makubwa yakujiendesha na kuchangia pato la Taifa, hivyo ni matumaini yangu makubwa kuwa bodi hii itasaidia shirika hili kutimiza malengo hayo na kusonga mbele zaidi," alisema Masauni.
Aidha, Waziri Masauni pia aliitaka Bodi hiyo aliyoizindua kutatua changamoto zilizopo, ambazo ni nikutokuwepo mfumo maalumu wa kujiendesha, kutozingatia kanuni na taratibu, kutokuwa na maono na nia ya dhati ya kujiendesha kibiashara na kutatua baadhi ya migogoro iliyopo.
0 Comments