Header Ads Widget

WADAU WA TAKSI WAKUTANA DAR ES SALAAM KUTOA MAONI (TAKSI MITA)

 


Na fatma Ally Matukio Daima APP Dar es Salaam 



Wadau wa taksi leo wamekutana jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kutoa maoni kuhusu mfumo mpya watakaotumia madereva wa taksi (Taksi Mita) kwenye magari yao ambao unatarajiwa kuanza mwakani wenye lengo la kumuwezesha abiria kuona bei halisi ya sehemu anayokwenda.


Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufungua Mkutano huo, Mkuu wa Wilaya ya Ilala Ludigija Ngw'ilabuzu amesema kuwa Serikali imedhamiria kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na kuongeza pato la taifa hivyo usafiri huo umekuwa ni wakuaminika hususani Dar es Salaam, hivyo wameona ni bora kuja na mpango mkakati ambao utaiboresha biashara hiyo.


Amesema kuwa, ni muhimu kwa wadau wa taksi Jijini Dar es Salaam kutoa maoni yatakayowezesha kuboresha usafiri wa taksi kwa manufaa yao na abiria wanaozitumia hususani taksi mita ambayo itawezesha abiria kutozwa nauli kwa haki.



"Rais Samia anataka kuona kila sekta inachangia pato la taifa hivyo wadau watoe maoni namna ya kuboresha na kutoa huduma hususani ya taksi mita ambayo ipo maeneo mengi duniani inasaidia kulinda mali na yule unaemwendesha ukisahau kitu kwenye taksi unaweza kurudi kukifuata"amesema Ludigija.


Hata hivyo, amesema fursa hiyo ambayo LATRA wameileta kwao ya kutoa maoni waitumie ili waweze kupata maoni bora ili kila mmoja anufaike bila kumuumiza mtu yeyote.


Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi LATRA Johannes Kahatano amesema magari ya kukodi kuwa na kifaa cha kuchakata nauli ni matakwa ya sheria hivyo maoni watakayotoa yatawezesha kuboresha utoaji huduma hiyo.



Aidha, amesema kuwa jambo hilo ni la watu wote na kubwa zaidi ni maoni kutoka kwao wanataka usafiri huo uweje na hata baada ya hapo wataendelea kupokea naoni hadi Desemba 31 mwaka huu kwa lengo la kila mtu aweze kutoa maoni yake Ili yafanyiwe kazi .


"Leo tunajadili maoni baada ya kukamilika kwa maoni hayo tutapanga nauli husika kwa kila umbali hivyo leo tutazungumzia vifaa vya kuchakata nauli peke yake"amesema Kahatano.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI