Header Ads Widget

NYONGEZA YA KIMA CHA CHINI CHA MSHAHARA NI AHUENI KWA VIJANA..

 


Na Gift Mongi,Matukio Daima App,Moshi


Mjumbe wa mkutano mkuu wa chama cha mapinduzi (CCM)mkoa wa Kilimanjaro Innocent Shirima amesema kiwango cha chini cha kima cha mshahara kilichotangazwa hivi karibuni na serikali kinaenda kuleta motisha kwa wafanyakazi na kuongeza mzunguko wa pesa mitaani.


Kwa mujibu Innocent ni kuwa nyongeza hiyo inaenda kuwagusa vijana walio wengi kwani wao ndio waajiriwa wengi  pia kupitia shughuli na huduma wanazozitoa wataweza kunufaika kutokana na hali ya kipato kwa wafanyakazi kuimarika.


Amesema kwa kipindi kirefu serikali ilikuwa haijagusa maslahi ya wafanyakazi jambo lililopelekea mzunguko mtaani kuwa mdogo japo kwa kipindi cha muda mchache rais Dkt Samia Suluhu Hassan alipoingia madarakani ameonesha nia yakuwakwamua wafanyakazi.


Shirima ameongeza kuwa kuongeza kiwango cha mishahara na madaraja ni kichocheo katika kuleta mafanikio na kuwa hapa ametengeneza mazingira ambayo yanaenda kumsaidia kijana kujiimarisha kiuchumi.


Anasema vijana walioajiriwa na wale waliojiajiri ni dhahiri pasipo na mashaka  kuwa serikali ya awamu ya sita imeonesha kuwajali na kuwaondolea kero zisizokuwa na msingi ikiwa ni pamoja na kuweka muongozo wa kima cha chini kwa walio katika sekta binafsi.


Shirima ambaye pia ni kamanda mstaafu wa chipukizi wilaya ya Moshi Vijijini anasema kwenye mambo yaliyo mazuri yanayofanywa kama hili la nyongeza ya mishahara halina budi  kupokelewa vyema na  kuendelea kuunga mkono jitihada mbalimbali zinazofanywa na serikali katika kuwaletea wananchi maendeleo.


Judith Matemu mkazi wa Marangu anasema kuongezwa kwa kima hicho cha mshahara kutawasaidia wengi na kutaongeza mzunguko wa fedha hasa kwa wale watu wa kima cha chini.


Anasema tuiombe serikali kima hiki kilichotangazwa kisiwe cha kwenye makaratasi pekee na badala yake serikali kupitia wataalam wake idara ya kazi kufuatilia na kuwachukulia hatua waajiri binafsi watakaokaidi muongozo huo.


Mapema mwezi huu serikali serikali imetangaza kiwango cha kima chini Kwa wafanyakazi waliopo kwenye sekta binafsi na kuwa kiwango hicho kinaenda kuanza kutumika rasmu mwezi januari 2023


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI