Header Ads Widget

MUTAFUNGWA, HATUHITAJI KUONA KITU KINAITWA DISKO TOTO KWENYE MKOA WETU.

 

NA CHAUSIKU SAID,MATUKIO DAIMAAPP MWANZA

Kamanda wa jeshi la polisi Mkoani Mwanza Wilbroad Mutafungwa amepiga marufuku  disko toto katika sikukuu ya Krismas na Mwaka Mpya.


Kauli hiyo ameitoa leo wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake na kueleza kuwa uwepo wa madisko hayo hupelekea msongamano usio wa lazima utakaoleta madhara Kwa afya ya watoto.


Mutafungwa amewataka wazazi/ walezi kuwa makini na kutowaacha watoto watembee peke yao bila uangalizi wa mtu mzima wakati wa sikukuu hizo.


" Sasa katika hilo wazazi tunaomba mtusaidie kuhakikisha watoto hawaendi kwenye mikusanyiko hiyo''Alisema Mtafafungwa.


Kwa upande mwingine ameeleza kuwa watumiaji wote wa Barabara wakiwemo watembea Kwa miguu, waendesha Baskeli, wasukuma guta na wanaotumia vyombo vya moto Kila mmoja Kwa nafasi yake ahakikishe anafuata sheria za usalama barabarani ili kuweza kuzuia ajali  zinazoweza kuepukika.


"Suala la ulinzi na usalama sio la vyombo vya usalama peke yake, Bali ni jukumu letu sote hivyo tunaomba wananchi tushirikiane Kwa kuchukua tahadhari za kiusalama ili tuweze kusherekea sikukuu Kwa usalama na kuukaribisha mwaka mpya 2023 tukiwa salama" amesema Mtufungwa.


Mutafungwa ameeleza kuwa Kuna baadhi ya watu ambao wanapenda kusherekea sikukuu Kwa kulipua baruti na kuchoma matairi ambapo vitendo hivyo vinachochea uvunjifu wa amani.


"Hatutakubali kuona barabara zetu zinachafuliwa Kwa sababu ya mtu mmoja ambaye anataka kumaliza mwaka Kwa kuchoma matairi hayo, wakae wakijua lokapu zetu zinawasubiri tutawaweka ndani sisi huku tunawasubiri" amesema Mutafungwa.


Aidha ametoa wito Kwa wananchi kuendelea kutoa taarifa za wahalifu na uhalifu ili kuhakikisha Mkoa wa Mwanza uko salama.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS