Header Ads Widget

MKURANGA NA TAASISI YA MWALIMU NYERERE WAFANYA SHEREHE YA MIAKA 61 YA UHURU WA TANGANYIKA



 Na Scolastica Msewa, Mkuranga

Wilaya ya Mkuranga kwa kushirikiana na Taasisi ya Mwalimu julias Nyerere wamefanya sherehe za maadhimisho ya miaka 61 ya Uhuru wa Tanganyika kwa kuongoza wananchi kuchangia damu na kufanya usafi katika hospitali na ofisi za serikali.


Maadhimisho hayo yaliyofanyika katika viwanja vya shule ya msingi Miteza Kata ya Njia nne wilayani Mkuranga na kuhusisha Kitengo cha damu salama na wadau mbalimbali wa maendeleo wilayani humo na Wazee wa kijiji hicho waliongoza shiriki kutoa mada mbalimbali za kuzungumzia masuala yaliyofanywa na Mwalimu Nyerere kijijini hapo katika utawala wake na hata siku ya tarehe 17 mwezi 2 mwaka 1973.


Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Khadija Nasiri Ally akizungumza na wananchi wa wilaya hiyo alisema waliamua kufanyia sherehe hizo za kumbukumbu ya miaka 61 ya Uhuru katika kijiji hicho kwakuwa kina historia kubwa na muhimu kwa kumbukumbu ya Rais wa Kwanza wa Tanzania Mwalimu Julias Kambalage Nyerere aliyofanya katika kijiji hicho cha Miteza wakati akiwa madarakani. 


Khadija aliwataka Vijana wilayani humo kuwa na moyo wa uzalendo kwa kufanyakazi kwa bidii na kujitolea ili kuijenga nchi yetu.


“Changamoto iliyopo sasa kwa vijana  wa Wilaya hiyo ni kukosa moyo wa uzarendo kwa kufanyakazi kwa bidii katika shughuli mbalimbali za maendeleo maana kama vijana wangekuwa na moyo wa kujitolea kasi ya maendeleo wilayani humo ingekuwa kubwa”  alisema.


Alisema Serikali inajitahidi kusimamia shughuli za maendeleo wilayani humo lakini jitihada za serikali zinakamilika kwa wananchi pia kujitokeza kwa wingi kushiriki utekelezaji wa shughuli hizo.


Katibu wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere mkoa wa Pwani Omary Pumzi alisema Taasisi hiyo iliamua katika kushiriki sherehe za kumbukumbu ya miaka 61 ya Uhuru washiriki kwa kuhamasisha wananchi kuchangia damu kwani mahitaji ni makubwa nchini.


Alisema walikuwa namalengo ya kupata damu chupa 200 ambazo zitasaidia wagonjwa katika hospitali za wilaya hiyo hasa kinamama wakati wa kujifungua.


Aidha Omary alihamasisha wananchi kuchangia damu ilikuhimalisha kiasi cha uhakika cha damu katika banki ya Damu salama nchini kwani hospitalini hakuna damu na mahitaji ni makubwa. 

Mkurugenzi wa Wiliaya ya Mkuranga Mwantumu Mgonja aliishukuru Serikali ya awamu ya sita kwa kuleta shilingi bilioni 2.64 kwaajili ya ujenzi wa madarasa 132 kwaajili ya wanafunzi wa kidato cha kwanza mwakani.


Mzee Juma Kindi (67) mzaliwa wa Miteza alipongeza serikali kwa hatua kubwa za maendeleo kuanzia utawala wa awamu ya kwanza hadi awamu hii ya sita kwani kijiji hiocho kimepiga hatua kubwa za maendeleo ikiwa ni pamoja na uboreshaji wa barabara za uhakika, kupatikana kwa shule ya msingi na sekondari na Zahanati. 





Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI