Header Ads Widget

MADEREVA WANAOSAFIRISHA KEMIKALI WAJENGEWA UWEZO WA KUKABILIANA NA MADHARA YA KEMIKALI.



*************************

Katibu Tawala Msaidizi Viwanda biashara na Uwekezaji mkoa wa Mwanza Patrick Karangwa , amefunga mafunzo ya siku mbili ya usimamizi wa kemikali kwa wasimamizi wa kemikali na madereva wanaosafirisha kemikali ambayo yalikuwa yakifanyika Jijini Mwanza .

Katibu Tawala Msaidizi Viwanda biashara na Uwekezaji mkoa wa Mwanza Patrick Karangwa amesema, ili kukabiliana na madhara yanayotokana na ongezeko la watumiaji na matumizi yasiyokuwa salama serikali inasisitiza kufuata sheria ya usimaminizi na udhibiti wa kemikali za viwandani.

Katibu Tawala Msaidizi Viwanda biashara na Uwekezaji mkoa wa Mwanza Patrick Karangwa amesema, kemikali zinafaida ngingi katika shughuli za wananchi za kila siku kwa uasilia wake lakini zinaweza kuleta madhara kwa afya na Mazingira wakati wa uzalishaji, usafirishaji, uhifadhi na utumiaji endapo hazitatumika katika hali ya usalama.

Mkurugenzi wa huduma za udhibiti wa Mamlaka ya maabara ya mkemia Mkuu wa Serikali Daniel Ndiyo amesema, kwa asilimia kubwa udhibiti umewezesha serikali kutambua aina za kemikali zinazoingia nchini mahali zinazopelekea na matumizi yake huku akisema wataendelea kuzuia kemikali hatarishi ambazo zinaweza kuleta madhara kwa wananchi na Mazingira.

Deogratius Runigangwe mshiriki wa mafunzo ya usimamizi wa kemikali kutoka Kampuni ya Barrick Bulyanhulu amepongeza utoaji wa mafunzo hay huku akisema yatawasaidia kwa kiasi kikubwa katika udhibiti wa kemikali.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS