Kufundisha kwa nyenzo na ubunifu mkubwa ni moja ya mkakati wa ufundishaji wa Elimu Bora katika shule za mkoa wa Pwani kutoa elimu Bora kwa wanafunzi wote mkoani humo ikiwa ni utekelezaji wa Mradi wa Shule Bora nchini.Mwandishi Scolastica Msewa anaripoti
KATIBU Tawala Mkoa wa Pwani Zuwena Omary ni miongoni mwa viongozi walioshuhudia mafunzo ya siku moja kwa Waandishi wa Habari Pwani huko Kibaha mkoani Pwani ambapo Walimu walitoa shuhuda namna wanavyofundisha kwa nyenzo na namna wanavyofundisha kwa ubunifu ili kurahisisha uelewa wa wanafunzi mashuleni.
Mradi huo wa Shule Bora wenye mpango mkakati kutoa elimu Bora kwa watoto wote nchini kwa wanafunzi rasmi wenye kulenga kuunga mkono Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuinua kiwango cha elimu jumuishi pamoja na kuweka mazingira salama ya kujifunzia kwa wanafunzi wote wa kike na kiume katika Shule za Serikali nchini.
Akifungua Mafunzo hayo Katibu Tawala huyo wa Mkoa wa Pwani
amewataka Waandishi wa Habari mkoani Pwani watumie Kalamu zao kwa weledi na uzalendo katika kuandika Habari za mradi wa Shule Bora ambao malengo yake ni kuboresha elimu nchini.
Amesema mradi huo ni wa ushirikiano kati ya serikali ya Tanzania na UK Aid mradi huu utafanya maboresho yatakayowezesha kila mtoto kupata msingi mzuri katika elimu yake ya awali , ili kuitumia fursa kwa kutoa mchango wake katika ukuaji wa nchi na maendeleo yake.
Amesema kuwa mradi huu ni kwa ufadhili wa serikali ya Uingereza kupitia mfuko wa UK Aid, gharama za mradi zitakuwa na bajeti ya Paundi za Kiingereza Mil.89 , sawa na Sh.za Kitanzania Bil.271 na utafanya kazi katika ngazi zote za mradi. Mradi huu wa Shule Bora utatekelezwa hadi ifikapo mwaka 2027.
Mradi huu wa Shule Bora una malengo manne ambayo ni kujifunza watoto wote watapata fursa ya kujifunza katika shule. Lengo.la pili ni Kufundisha mfuko wa msaada wa UK Aid utaunga mkono na kuimarisha kazi ya ufundishaji nchini.
Lengo la tatu Jumuishi ambapo itahakiki sha kuwa watoto wote wa kitanzania mashuleni wanakuwa katika mazingira salama na rafiki ili kuwa wezesha kumaliza elimu ya msingi na wana endelea na elimu ya Sekondari na lengo la nne ni kujenga mfumo UK Aid utaunga mkono serikali na kuimarisha ili kupata au kuwa na thamani ya fedha katika utoaji wa elimu katika ngazi zote toka chini hadi ngazi ya taifa.
0 Comments