Header Ads Widget

FAINALI ZA MBIO ZA MITUMBWI ZAFANYIKA JIJINI MWANZA

 





Fainali za mashindano ya mbio za mitumbwi ( Tanzania botrace ) yamefanyika jijini Mwanza katika soko la kimataifa la samaki huku jumla ya timu 32 za wanawake  12 na wanaume 20 zimeshiriki mbio hizo ambazo zimekuwa na ushindani mkubwa.


Mratibu wa mbio za mitumbwi Tanzania botrace Scope Solution Benard Matta amesema mbio hizo zimekuwa na fursa katika kutangaza mbio hizo ndani ya mikoa ya kanda ya ziwa zikiwemo na wilaya zake kupitia sekta zote za kimaendeleo kama afya,utalii,viwanda,ajila na uvuvi endelevu. 

Dkt Ayub Sossy Meneja wa Scope Kanda ya ziwa amesema, wanatarajia kupanua wigo wa Mashindano ya Tanzania Botrace ndani ya kanda ya ziwa na nje ya kanda ya ziwa kama vile ziwa Tanganyika ,Ziwa Nyasa na Bahari ya Hindi kwa malengo ya kutangaza na kufungua milango kwa wawekezaji kutoka ndani na nje ya nchi.

Akizungumza kwa niaba ya washiriki wengine wa mashindano ya mbio za mitumbwi Tanzania Bot race mwaka 2022 Sikitu Daud ambaye pia ni mshiriki wa mbio hizo ameyapongeza mashindano hayo huku wakiomba mwakani yaweze kuboreshwa zaidi kwa kupewa sare za tshart  kama ilivyokuwa miaka mingine yote

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI