Bodi ya wadhamini mfuko wa misitu Tanzania imetembelea chuo Cha mafunzo ya viwanda vya misitu ( Fiti) Moshi kwa lengo la kukagua na kujionea miradi mbalimbali iliyofadhiliwa na mfuko huo .
Aidha miradi iliyofadhiliwa ni pamoja na Ujenzi wa wa jengo la maabara , maktaba ,ununuzi wa vifaa vya maabara, vifaa vya maktaba , pamoja na ununuzi wa basi dogo(mini bus) kwa matumizi ya wanafunzi wa chuo wakiwa katika mafunzo,pamoja na kugharamikia utengenezaji wa samani na bidhaa nyingine kutokana na mabaki ya mbao na miti.
Akizungumza katika ziara hiyo Tuli Msuya Mtendaji Mkuu wa mfuko wa misitu Tanzania ambaye pia ni Katibu wa bodi ya wadhamini mfuko wa misitu Tanzania amesema kuwa lengo la ziara hiyo ni kutembea chuo hicho cha FITI Moshi kwa la kujionea jinsi mfuko wa misitu Tanzania ulivyochangia katika kuboresha mazingira ya chuo kwa maana kwamba ufundishaji na Mazingira ya kujifunzia.
Amesema kuwa mfuko wa misitu Tanzania umeanzishwa kwa lengo la kuwa chanzo Cha Muda Mrefu na endelevu Cha fedha kwa ajili ya kuwezesha uhifadhi na usimamizi,na uendelezaji wa usimamizi wa rasimali za misitu.
"Huu mfuko unawezesha vyuo vyote ambavyo vipo chini ya idara ya misitu na nyuki ambayo pia idara ipo chini ya wizara ya maliasili na utalii ikiwemo chuo Cha misitu ambacho kipo olmotonyi ,chuo Cha mafunzo ya wafugaji nyuki ambacho kipo tabora,."Alisema
Hata hivyo ametoa Rai kwa chuo hicho cha FITI kuhakikisha kwamba wanasimamia rasilimali Zilizopo kwa kuhakikisha wanazitunza na kuzichukulia Kama Chachu ambayo inawezesha kuboresha elimu inayotolewa chuoni hapo.
"Kwa hiyo natoa wito waendelee kulitumza na pindi inapotokea Kuna changamoto ndogo ndogo za uharibifu wajitahidi kufanya marekebisho mapema ili iweze kudumu kwa Muda mrefu na tuendelee kutoa mafunzo hapa chuoni"Alisema.
Kwa upande wake Mkuu wa chuo hicho cha viwanda vya misitu Fiti Dct. Joseph Makero amesema kuwa lengo la bodi wa mfuko wa misitu Tanzania imetembelea kuja kuangalia miradi ambayo chuo kimetekeleza kwa kipindi Cha miaka 8 kuanzia mwaka 2014 mpaka mwaka 2022.
"Chuo katika kipindi hicho kilipata miradi mitano ikiwemo Ujenzi wa jengo jipya, maktaba na maabara ambayo kwa kweli limechagiza sana mazingira ya chuo na imeongeza miundombinu ya mazingira mazuri ya kujifunzia wanafunzi wetu" Alisema.
Sambamba na hayo amesema kuwa mradi mwingine walioutekeleza ni pamoja na mradi wa kuongeza thamani mazao ya mbao inayoutea (finger joints).
Na mradi huu tuliibua kwa lengo la kwa lengo la kutekelezwa ilani ya chama Cha mapinduzi ambayo pia ilikuwa inataka jamii iweze kutumia mabaki ya mbao kwa ajili ya kuitengenezea bidhaa mbalimbali za mbao na pia kupunguza upotevu wa Mali ghafi za miti "Alisema.
Hata hivyo amesema kuwa wao kama chuo wataendelea kushirikiana na mfuko wa misitu kwa ajili ya kuibua miradi mingine na kutekeleza vizuri miradi na kutunza na kuhifadhi rasilimalia za misitu.
0 Comments