NA HAMIDA RAMADHAN DODOMA
WAZIRI wa Elimu Profesa Aldof Mkenda amesema Serikali kupitia Wizara hiyo ipo mbioni kuanzisha mfuko rasmi wa kuwasaidia waandishi mahiri wa vitabu huku akiwataka waandishi wote nchini kuchangamkia fursa zinazotolewa ili kutoa maaandiko makini yatakayoleta tija kwenye jamii.
Aliyasema hayo Jijini Dodoma alipokuwa akimuwakilisha Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwenye ukizundua wa kitabu cha Continuity with Vision the Roadmap to Success for President Samia Suluhu Hassan .
Waziri Mkenda alisema katika uongozi wa Rais Samia uongozi umuhimu wa uandishi umeonekana na Serikali kuona haja ya kufanya kwa vitendo kwa kuanzisha tuzo ya Mwalimu Nyerere ili waandishi nguli na mahiri kuweza kushiriki na kujipatia tuzo hizo
Pia Waziri Mkenda aliipongeza ESAURP kwa uandishi na uchapishaji wa vitabu vingi ambavyo vimekuwa vikifundisha na kuelimisha jamii
" Katika kitabu hiki nimeona kimeandikwa na waandishi wengi na ndani yake kunavitu vingi Mimi nitajikita katika kurasa wa 11 Masuala ya elimu
Kwa upande wake Mwandishi wa kitabu hicho Profesa Ted Maliyamkono Alisema Kulikuwa na kila sababu ya kuandika kitabu hicho kwa kushirikisha watu mbalimbali ili kuwaeleza watanzania na dunia kwa ujumla mambo mengi na mazuri yanayofanywa na Rais wa awamu ya sita Samia Suluhu Hassan.
Alisema katika kitabu hicho walizingatia mambo muhimu ya Kisera na sio kufanya tathmini ya utawala wake na kuwataka wananchi wasione udhaifu wa kitabu.
Vilevile alitaja lengo kuu la chapisho hilo kuwa ni kuchangia uboreshaji wa Sera serikalini.
"Ndani ya kitabu hiki kinaonyesha Rais Samia amekuwa wa kwanza kutembelea nchi nyingi tofauti na wengine ili kufungua njia zilizofungwa na milango ya biashara,pia amekuwa Rais wa kwanza kufanya Royal tour na amekuwa Mtendaji wa vitendo na sio wa maneno," Alisema Mwandishi huyo wa kitabu
Aidha alisema katika utawala wake Rais Samia amekuwa Rais wa kwanza kuteua mawaziri wawili Wanawake katika Wizara mbili ambazo hazikuwahi kuongozwa na mwanamke enzi na enzi ambazo ni Wizara ya Ulinzi na Wizara ya Mambo ya Nje.
"Rais Samia pia ameendeleza kazi yote iliyoachwa na Rais wa awamu ya tano hayati John Magufuli na kuhakiki Katiba mpya na kuona atashughulikia kwa namna gani na kwa wakati ulio sahihi,"alisema
Naye mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule alisema kitabu cha Continuity with Vision the Roadmap to Success for President Samia Suluhu Hassan kinakwenda kujibu maswali ya Watu wengi na makundi mbalimbali kuhusu hoja nyingi zilizomo kwenye jamii.
Alisema kitabu hicho kimetumia muda mchache kuandikwa kutokana na ukweli kwamba Rais wa awamu ya Sita amekuwa Mtendaji kwani kwa Kipindi kifupi ameweza kufanya mengi.
Awali akiongea katika Uzinduzi huo mkuu wa chuo cha Mipango na Maendeleo Vijijini Profesa Hozen Mayaya alisema Rais ametekeleza kwa ufanisi miradi ya kimkakati na kutolea mfano ushiriki wa filamu ya Royal tour ambao umeongeza idadi ya watalii wanaokuja kutembelea nchini na kazi kubwa ya wananchi ni kuendelea kumuombea.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Umoja wa Vyuo vya Mashariki na Kusini mwa Afrikia ( ESAURP) Ruta Mutakyawa alitumia nafasi hiyo kusema kuwa walisimamia uandishi na uchapishaji wa kitabu hicho ambapo kitabu kina kurasa 624 ,sura 29.
Alieleza kuwa kitabu hicho kimewashirikisha Watu 45 waliotoka vyuo vya elimu ya juu, mashirika ya umma na asasi za kiraia.
0 Comments