Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Mhandisi Kundo Mathew akizungumza katika ziara ya kukagua miundombinu ya miradi ya mawasiliano na usikivu wa TBC katika Wilaya ya Ludewa, Mkoa wa Njombe.
Matukio katika picha: Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Mhandisi Kundo Mathew akiwa katika ziara ya kukagua miundombinu ya miradi ya mawasiliano na usikivu wa TBC katika Wilaya ya Ludewa, Mkoa wa Njombe.
Matukio katika picha: Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Mhandisi Kundo Mathew akiwa katika ziara ya kukagua miundombinu ya miradi ya mawasiliano na usikivu wa TBC katika Wilaya ya Ludewa, Mkoa wa Njombe.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Na Immaculate Makilika – MAELEZO, Ludewa
Naibu
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Mhandisi Kundo
Mathew amekagua vifaa vya ujenzi wa mnara wa mawasiliano utakaojengwa na
Kampuni ya Mawasiliano ya Simu za Mkononi ya Tigo katika Kijiji cha Nkwimbili Wilaya ya Ludewa, Mkoa wa Njombe.
Ambapo
baadhi ya vifaa alivyokagua ni pamoja na nondo, taa za mnara, miguu ya mnara,
jenereta, mtambo wa kudhibiti umeme na betri.
Akihutubia
wananchi Novemba 27, 2022 katika Kijiji cha Lupingu wilayani humo, Mhe.
Naibu Waziri Kundo amesema kuwa lengo la kutembelea mradi huo ni kujua
utakamilika lini na huduma watakazopata wananchi.
“Ifikapo
Januari 2023 mnara huu utaanza kutoa huduma kwa wananchi na hivyo kutatua
changamoto ya mawasiliano katika eneo hili. Wizara tuna miradi ya mipakani na
maeneo maalum ili kuhakikisha wananchi wanapata mawasiliano kutoka nchini
kwanza ikiwa ni pamoja na kuchangia uchumi wa nchi kwa manufaa yetu sote”,
ameeleza Mhe. Naibu Waziri Kundo.
Hata
hivyo amewataka wananchi kuendelea kutoa ushirikiano wakati wa ujenzi wa mradi
huo pamoja na kuulinda mara utakapoanza kutoa huduma, huku akiwasii kutumia
vizuri fursa za mawasiliano watakazopata kutokana na mnara huo.
Kwa
upande wake, Msimamizi wa Mradi wa ujenzi wa mnara katika Kijiji cha Nkwimbili
kutoka Kampuni ya GNC Solutions LTD, Bw. Suleiman Senga ameahidi kuwa mnara huo
utaanza kutoa huduma ifikapo Januari 2023 na kuwa kampuni zingine za simu
zinaweza kutumia mnara huyo wa Kampuni ya Tigo kutoa huduma kwa wananchi
kupitia kampuni zao.
Kuhusu
mnara wa TBC uliopo Milo wilayani humo, Mhe. Naibu Waziri Kundo amesema kuwa
kupitia mnara huo vituo vya vingine vya redio vinaruhusiwa kuweka vifaa vyao
ambavyo vitasaidia kuongeza usikivu wa matangazo yao.
Katika hatua nyingine, Mhe. Naibu Waziri Kundo ameielekeza Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kuhakikisha kuwa wanazingatia utaratibu na kuzisaidia kupata leseni kwa haraka redio mbalimbali zilizowasilisha maombi yao ikiwa ni pamoja na redio za halmashauri.
0 Comments