Header Ads Widget

MABINTI MAZINGIRA MAGUMU MUFINDI WAPEWA MAFUNZO YA KUTHIBITI MOTO



NA FRANCIS GODWIN,IRINGA. 

HALMASHAURI ya wilaya ya Mufindi mkoani Iringa Kwa kushirikiana na mradi wa Youth Agency Mufindi (YAM) imetoa mafunzo ya uthibiti wa moto Kwa wasichana toka mazingira magumu wa mradi huo kutoka vijiji 16 kata za Ihanu, Mdabulo na Luhunga.


Akizungumza jana wakati wa mafunzo hayo Mkufunzi wa mafunzo Walter Mushi alisema mafunzo hayo yatawasaidia mabinti hao kusaidia kuthibiti moto pindi wanapokuwa Katika shughuli zao za Kilimo Cha mazao ya misitu kama Miti .


Kwani alisema kupitia mafunzo hayo washiriki wamepatiwa elimu ya kutosha ya kukabiliana na majanga ya moto pindi yanapotokea Katika maeneo yao .


"Wilaya ya Mufindi ni wilaya inayofanya vizuri Katika Kilimo Cha miti hivyo mafunzo haya Kwa mabinti hawa ni moja kati ya mafanikio ya kukabiliana na majanga ya moto yanapojitokeza" alisema 


Kupitia mafunzo hayo washiriki wamejifunza uzimaji wa moto aina mbali mbali ukiwemo moto wa ardhini na angani bila kuleta madhara makubwa zaidi .



Alisema Serikali iliyopo madarakani chini ya Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na Dunia ipo Katika harakati ya kukabiliana na Mabadiliko ya tabia Nchi yanayosababishwa na kasi ya uharibifu wa mazingira ikiwemo ya moto Kichaa .


"Mabinti hawa mradi wa YAM Watakuwa mabalozi wazuri kwenye vijiji vyao na watakuwa msaada mkubwa Kwa kuthibiti majanga ya moto na Kwa hili Mradi wa Youth Agency Mufindi ni ukombozi mkubwa "


Huku washiriki wa mafunzo hayo wamepongeza mradi wa YAM Kwa kuwateua kushiriki mafunzo hayo na kuahidi kiyatumia mafunzo hayo kuleta matokeo mazuri ya uthibiti wa moto Katika maeneo yao .


Mkuu wa wilaya ya Mufindi Saad Mtambule akizungumza juu ya faida ya mafunzo hayo na jitihada za mradi wa YAM alisema Serikali inajivunia kuona jitihada hizo .


Kuwa mafunzo Kwa mabinti hao yatakuwa na tija kubwa Kwa wilaya ya Mufindi ambayo sehemu kubwa imezungukwa na misitu ya Serikali na misitu binafsi .


Meneja mradi wa YAM Zilipa Mgeni alisema mafunzo hayo yanatolewa Kwa vijana 50 ambao wamegawashwa kwenye vikundi vitano vya mabinti 10 Kila kikundi na wamekuwa wakipewa mafunzo tofauti tofauti .


Mafunzo yanayotolewa ni pamoja na  Mbinu ya upandaji miti na usimamizi Bora ,mbinu za uvunaji na usimamizi wa msumeno ,uchakataji mbao ,uoteshaji miti ,utengenezaji mkaa wa Pumba za miti na kozi nyingine nyingi .


Mradi wa Youth Angency  Mufindi  unatekelezwa na Halmashauri ya Mufindi chini ya mradi wa Foxes  Community and Wildlife Conservation( FCWC) na YAM kupitia ufadhili wa Finland unatekelezwa kwenye kata za Luhunga ,Ihanu na Mdabulo ni mradi utanufaisha  vijana na  watoto  wanaotoka  katika  familia duni zaidi ya   vijana 770  katika  vijiji 16.





Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI