Header Ads Widget

ANNE KILANGO CUP TARAFA YA GONJA YAHITIMISHWA LEO KWA KLABU YA MAFINGIRO KUIBUKA BINGWA WA MASHINDANO HAYO.

 


NA WILLIUM PAUL, SAME.


KLABU ya Mafingiro kutoka kata ya Mtii imeibuka bingwa katika ligi ya Anne Kilango Cup Tarafa ya Gonja baada ya kuifunga klabu ya Ntenga kutoka kata ya Vuje kwa mikwaju ya penati 3 kwa 2 baada ya kutoka sare ya magoli matatu ndani ya dakika 120.



Fainali hizo zilizochezwa leo katika uwanja wa Ngaeni kata ya Mtii Jimbo la Same Mashariki wilayani Same mkoani Kilimanjaro ambapo mashindano hayo yaliyoshirikisha klabu 12 yamedhaminiwa na Mbunge wa Jimbo la Same Mashariki, Anne Kilango Malecela.



Mabingwa hao wa Anne Kilango Cup walijishindia kiasi cha fedha taslimu Milioni 1, medali, seti ya jezi, mpira pamoja na kombe huku mshindi wa pili, Ntenga akipata zawadi ya fedha taslimu laki nane (800,000), pamoja na jezi, medali na mpira, huku mshindi wa tatu ambaye ni Bombo Fc kutoka kata ya Bombo akiambulia fedha taslimu laki sita (600,000), jezi, mpira pamoja na medali.



Akizungumza mara baada ya kukabidhi zawadi hizo, Mbunge wa Jimbo la Same Mashariki, Anne Kilango Malecela alisema kuwa, lengo la kuanzisha mashindano hayo ni kuwaweka pamoja vijana wa jimbo bila kujali itikadi za vyama vyao.



Mbunge huyo alisema kuwa, ameamua kuanzisha mashindano ya kitarafa ili kupata timu moja ya Tarafa ambapo wachezaji hao watatengeneza timu ya Jimbo itakayoenda kushindana na timu ya Waziri Mkuu Kasimu Majaliwa Majaliwa.


Alisema kuwa, michezo kwa sasa ni ajira hivyo yeye kama Mbunge ameamua kuinua vipaji walivyonavyo vijana na kuvitangaza huku pia akiitaka klabu ya Polisi Tanzania na

klabu nyingine zinazoshiriki ligi kuu Tanzania Bara na pamoja na ligi za chini kufika katika jimbo hilo klujionea vipaji na kupata wachezaji watakaowatumia.


“Toka kuanza kwa mashindano haya Tarafa ya Mamba vunta na leo fainaili Tarafa ya Gonja tumeona vijana wakionyesha vipaji vyao hivyo niziombe klabu za ligi kuu Tanzania bara kuja kujionea wenyewe vipaji wapo wachezaji wakubwa huku ila hawajapata sapoti ya kwenda mbele” alisema Mbunge Anne Kilango.



Aidha Mbunge huyo alitumia nafasi hiyo kuwaomba vijana kulinda Jimbo na kata zao pamoja na kumlinda Rais Samia Suluhu Hasani kwa kufanya kazi kwa bidii pamoja na kuunga mkono juhudi mbalimbali zinazofanywa na Serikali.


Kwa upande wake, Mgeni rasmi katika mashindano hayo ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Same, Edward Mpogolo alitumia nafasi hiyo kumpongeza Mbunge Anne Kilango kwa dhamira yake ya kuanzisha mashindano hayo ikiwa ni kuonyesha jinsi anavyowathamini vijana wa Jimbo la Same Mashariki.



Mpogolo alisema kuwa, michezo hiyo inatoa fursa kwa vijana kuwa wamoja na kuwajenga kuwa na ushirikiano ambapo imekuwa ikiwakutanisha vijana kutoka katika maeneo mbalimbali.


Alisekuwa kuwa. Mbunge Anne Kilango ameonyesha kufanana na Rais Samia Suluhu Hasani kwa namna ambavyo anahamasisha michezo ambayo inawaunganisha vijana.



Aidha michezo hiyo imekuwa ikitumika kuhamasisha vijana kutunza wa mazingira kwa kupanda miti pamoja na kuhamasisha vijana kufanya kazi ili kujipatia kipato.


“Mbunge ameonyesha dhamira yake ya dhati ya kutunza vipaji vya vijana leo hii michezo imekuwa ni sehemu ya ajira hivyo anavyowakusanya vijana pamoja wapo watakaoonwa na klabu mbalimbali ikiwamo Polisi Tanzania” alisema Mpogolo.



Mkuu huyo wa wilaya aliongeza kuwa, michezo hiyo pia imekuwa ikichangia vijana kuwa na maadili mema na kuacha katika makundi maovu ya uvutaji bangi pamoja na vijiwe vya pombe.


Mwishoo..

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI