Header Ads Widget

9.1% YA VIFO VITOKANAVYO NA UGONJWA WA KISUKARI.

Kaimu meneja mpango wa kuthibiti magonjwa yasiyoambukiza Valeria Millinga
Katibu Tawala Wilaya ya Misungwi Petero Sabato
Mwenyekiti wa chama Cha sukari Tanzania prof. Andrew swai

                        xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

NA CHAUSIKU SAID,MATUKIO DAIMAAPP MWANZA.

Vifo vitokanavyo na magonjwa  yasiyoambukiza vinachangia takribani asilimia 33 hapa Nchini huku ugonjwa wa kisukari ukiwa ni 9.10%


Hayo yamesemwa na Kaimu Meneja Mpango wa Kudhibiti Magonjwa Yasiyoambukiza Valeria Milinga kwenye madhimisho ya siku ya Kisukari Duniani ambayo Kitaifa yamefanyika Wilaya ya Misungwi Jijini Mwanza. 


Millinga ameeleza kuwa kutokana na Tafiti zilizofanyika katika halmashauri 50 hapa Nchini ambapo katika Nchini kumi(10) zinazoongoza Kwa ugonjwa wa kisukari Barani Afrika huku Tanzania ikiwa nafasi ya nane.


"Katika kuongeza uhamasishaji na uelewa kwa wananchi juu ya magonjwa  yasiyoambukiza hasa ugonjwa wa kisukari tumeweza kufanya maonyesho ya wiki ya magonjwa yasiyoambukiza yaliyoanza tarehe 5-12, Novemba 2022 ambayo yanafanyika kila mwaka." Amesema Bi. Milinga 


Aidha, Milinga ametaja mafanikio ya maonyesho hayo kwa mkoa wa Mwanza hadi kufikia siku ya kilele tarehe 12, Novemba, 2022 wananchi takriban 3000 wamejitokeza kupima ugonjwa wa Kisukari na 34 kati yao wamegundulika kuwa na ugonjwa huo.


Hata hivyo, amebainisha mafanikio waliyoyapata katika utoaji wa huduma za kisukari ikiwemo upatikanaji wa Dawa, utoaji wa mafunzo kwa watoa huduma za Afya katika Vituo 300 kwenye Mikoa 9.


Kwa upande wake Katibu Tawala wa Wilaya ya Misungwi Petero Sabato ambaye alikuwa Mgeni rasmi katika maadhimisho Hayo ameeleza kuwa Watanzania wanahitaji elimu zaidi ili waweze kuepukana na magonjwa yasiyoambukiza ikiwemo ugonjwa wa Kisukari ambao umekua ukiongezeka nchini.


"Elimu inahitajika zaidi ili kuwakinga wananchi na Magonjwa Yasiyoambukiza hasa Kisukari kwa kuwa ugonjwa wa Kisukari umekua ukigharimu maisha ya watu ikiwa ni pamoja na kukatwa baadhi ya viungo ." Amesema Sabato


Sabato ametoa rai kwa wananchi kufanya mazoezi sambamba na kupima Afya angalau mara moja kwa mwaka ili ukigundulika mapema inakuwa rahisi kupata matibabu.


Naye, Mwenyekiti wa Chama cha Kisukari Tanzania Prof. Andrew Swai amesema miaka ya 1991 kulikuwa na 1% tu ya ugonjwa wa kisukari nchini lakini kwa sasa imeongezeka hadi kufikia 9%.


"Kutokana na ongezeko la ugonjwa wa kisukari nchini imekua tatizo ambapo inagharimu 20% ya bajeti ya Serikali ili kuwahudumia wagonjwa hao." Amesema Prof. Swai


Baadhi ya wagonjwa wa kisukari wameeleza kuwa serikali Ina haja ya kuendelea kutoa elimu Kwa jamii ili wawe na tabia ya kupima magonjwa yasiyoambukiza.


" Bado jamii nyingine hazina uelewa juu ya magonjwa haya na inapotokea mtu anaumwa magonjwa haya hawaendi kwanza hospital wanakimbilia kwenye dawa za kienyeji" Walisema.


Maadhimisho hayo yameandaliwa na Wizara ya Afya kwa kushirikiana na wadau wa Chama cha Kisukari Tanzania (TDA), Shirikisho la Vyama vya Magonjwa Yasiyoambukiza (TNCDA) na viongozi wa Mkoa wa Mwanza wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya.








Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS