Header Ads Widget

WATU 10 WAJERUHIWA KWA MAPANGA NA KUPORWA MALI ZAO-MKURANGA PWANI

 


Watu kumi wamejeruhiwa na kundi la watu wasiojulikana  baada ya kuvamia nyumba nane huku wakikatwa mapanga usiku wa kuamkia leo katika Kijiji cha Tambani wilayani mkuranga mkoa wa Pwani.

Baadhi ya wananchi waliojeruhuwa katika tukio Hilo Fatuma Kamisi Alisema kuwa watu hao walivamia usiku na kuvunja milango na kudai wanataka pesa na simu.

"Walivunja mlango nilikuwa na mume wangu wakidai wanataka pesa wakachukua shilingi laki moja  na simu na kuniachia majeraha katika.mkono wangu wa.kushoto 

Naye Ramadhani Kipengele Alisema kuwa walivyoingia ndani  walikuwa wanadai simu na pesa hapakuwa na purukushani yeyote Ile lakini walinipiga na panga na wakaondoka na simu na pesa, 



kwa upande wake mwenyekiti wa Kijiji hicho Hilaly Komba amekiri tukio Hilo na kusema baada ya kupata Taarifa kutoka kwa wananchi waliwasiliana na jeshi la Polisi na wameshukuru jeshi Hilo kufika katika eneo la tukio.

"tunashukuru Kamanda wa Polisi mkoa wa kipolisi Rufiji amefika na kuwapa pole wajeruhi waliopatwa na tukio Hilo huku akiomba msaada wa kukamilika kwa jengo la kituo Cha polisi kilichojengwa kwa nguvu za wananchi mpaka kufikia hatua ya Renta hivyo itasaidia kuongeza ulinzi katika maeneo hayo." Alisema Komba

katika Kijiji hiki tunakuwa na vikundi vya ulinzi shirikishi ambavyo wananashiriki kulinda kwa muda lakini kwa Sasa wananchi walipumzika Sasa ndio tukio Hilo limejitokeza hivyo tutaanza Tena zoezi hilo.alisema Komba.



Naye kaimu kamanda wa Polisi Mkoa wa kipolisi Rufiji ambaye ni kamishina msaidizi wa jeshi la Polisi Protus Mutayoba amekiri kutokea kwa tukio Hilo na kujionea Hali halisi ya majeruhi na kuwaagiza viongozi wa vijiji kuanzisha vikundi imara vya sungusungu,ulinzi shirikishi ili kukabiliana na matukio hayo.

Kutokana na matukio haya ambayo hayakubaliki katika jamii nawaagiza viongozi wa vitongoji kutokulala na kufanya kazi kwa ushirikiano katika kuanzisha vikundi vya ulinzi shirikishi kwa ajili ya ulinzi wa amani katika maeneo haya".Alisema Mutayoba.

Pia kamanda Mutayoba alifika katika jengo la Polisi lililojengwa kwa nguvu za wananchi na kujionea namna ujenzi unavyoendelea na kuahidi kuwasaidia ili eneo hilo liweze kuwa na kituo Cha polisi Hali itakayosaidia wananchi kutumia muda na kupunguza adha ya kutumia umbali mrefu kufuata huduma ya Polisi.

Jeshi la Polisi mkoa wa kipolisi Rufiji linaendelea na kazi katika eneo hilo ili kuweza kuwabaini watu wanaovunja amani na kurudisha nyuma shughuli za maendeleo kwa wananchi.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS