Header Ads Widget

SERIKALI YAHIMIZA MATUMIZI BORA NA SALAMA YA MITANDAO



NA MWANDISHI WETU, ZANZIBAR –MATUKIO DAIMA APP

 Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknologia ya Habari imehimiza matumizi bora na Salama ya Mitandao ili kuhakikisha Maudhui Mitandaoni yanaendelea kuwa yenye Manufaa kwa watumiaji wote sambamba na kuhakikisha Makosa ya Uvunjifu wa Sheria za Mitandao yanapungua kwa kiasi kikubwa.

 

Wito huo umetolewa na Mkurugenzi Msaidizi wa Usalama Mtandao, Mhandisi Stephen Wangwe kwa vijana eneo la Forodhani Mjini Magharib Unguja ikiwa ni muendelezo wa ziara yake maalum ya kutoa Elimu juu ya Usalama wa Mtandao kwa Makundi mbalimbali.

 

Mhandisi Wangwe amesema ni vyema kwa Vijana na Makundi mengine kutumia vyema mitandao ili kuchangia ukuaji wa Uchumi na kuepuka matumizi yanayokiuka sheria kanuni na Maadili ya Nchi.

 

Amesema, Vijana wanapaswa kuwa Mstari wa mbele katika kuhakikisha Matumizi bora na Salama ya Mitandao yanafikiwa ili kuepusha uhalifu  pamoja na udhalilishaji mitandaoni.

 

“Tunaendelea kuhamasisha kwa Vijana na Makundi mengine katika jamii kuwa na Matumzi mazuri ya Mtandao kutokana Makosa ya kimtandao yamekuwa yakiongezeka kila Kukicha,” amesema.

 


Katika Maelezo yake Mhandisi Wange ameeleza namna alivyofarijika na mapokezi ya Elimu ya Usalama wa Mtandao yalivyopokelewa na na Vijana wa Makachu Forodhani.

 

“Sisi Binafsi kama Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari tumefarijika kwa kiasi kikubwa mara baada ya kufika katika eneo hili la Forodhani na tumepokewa vyema na vijana hawa ambapo tumewapa Elimu juu ya Usalama mtandao na wameipokea vizuri,” Ameeleza.

 

“Matumaini yetu kuwa Elimu hii itafika mbali zaidi kutoka na Vijana hawa kuwa maarufu lakini pia kwa namna ambayo wameipokea elimu hii, hivyo nitoe wito sasa kwa taasisi mbalimbali za Serikali na Binafsi kupokea Positive Elimu hii ya Usalama wa Mtandao na kuelimisha wengine,” ameongeza Kueleza.

 

Mhandisi Wangwe ametoa rai kwa vijana hao eneo la Forodhani  kuwa Mabalozi wazuri kwa Vijana wengine ili Elimu ya Usalama wa Mtandao inawafika vijana wengi zaidi na kutimiza wajibu wa kufaya aga ya Mtandao kuwa Salama zaidi.

 

Hata hivyo ametoa Wito kwa jamii kuwa na muamkoa wa kuripoti kwa polisi matukio ya uhalifu wa imtandao yanpotokea ili kuwezesha wengine wasifikiwe na Majanga ya Uhalifu wa Kimtandao.

 

“Mimi nitoe Wito kwa Wazanzibar wote wame na tabia ya kuripoti Polisi wanapotokezewa na Majanga ya Kimtandao ili yafanyiwe kazi na tuwe na takwimu sahihi lakinu pia kuwezesha wale wengine ambao hawajafikiwa na majanga haya kuepuka kufikiwa,”Amefafanua.

 

Katika ziara hiyo  Mkurugenzi  Msaidizi wa Usalama wa Mtandao ameambatana na maafisa mbalimbali kutoka Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari huku kauli mbiu ya Mwaka huu ya Usalama wa Mtandao ikisema ‘ USALAMA WA MTANDAO HUANZA NA MTU BINAFSI’.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS