Header Ads Widget

SERIKALI YAAHIDI KUTOA USHIRIKIANO KWA WAWEKEZAJI

 




Fatma Ally Matukio Daima APP Dar es Salaam


Serikali imesema imedhamiria kufanya mapinduzi makubwa katika kuwalea wawekezaji kutoka ndani na nje ya nchi kwa kupunguza kiasi cha fedha anachotakiwa kulipa mwekezaji Ili aweze kujisajili katika kituo cha uwekezaji (TIC).


Kauli hiyo, imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Waziri wa Uwekezaji Viwanda na Biashara Dk Ashatu Kijaji wakati akizindua jukwaa la biashara kwa wawekezaji lililowaunganisha wafanyabiashara wa Tanzania na Italia.


Aidha, amesema mpaka sasa uwekezaji wenye Thamani ya dola bil 2 za kimarekani umeshafanyika nchini Tanzania kutoka kampuni za Italia, huku akiwataka watanzania kutoa maoni kuhusu maboresho ya sheria mpya ya uwekezaji Ili mazingira yawe rafiki zaidi kwa wawekezaji wote.



Kwa upande wake, Balozi wa Tanzania nchini Italia Mahmoud Thabiti Kombo amewataka watanzania hususani wafanyabiashara kujitokeza kwa wingi kuchangamkia fursa za kibiashara zilizopo kutoka kampuni za nje hususani zinazotoka Italia kwani kwa sasa wamekuwa wawekezaji wazuri nchini Tanzania.


Aidha, amewataka watanzania kuchangamkia fursa mbalimbali zinazotolewa na Serikali ikiwemo fursa zinazopatikana kupitia filamu ya Royal Tour, pamoja na kushiriki katika kupeleka bidhaa mbalimbali nchini Italia ikiwemo ngozi .


Naye, Balozi wa Italia nchini Tanzania Marco Lumbardi amesema kuwa mashirikiano ya kibishara yalipo kati ya Tanzania na Italia ni ya muda mrefu ambapo dola bill 2 za kimarekani wamewekeza nchini Tanzania kupitia kampuni zao mbalimbali zilizopo nchini Tanzania, hivyo ameahidi kudumisha mahusiano hayo.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI