Header Ads Widget

SAHARA SPARKS KUWAKUTANISHA VIJANA WABUNIFU

 


Na fatma Ally Matukio Daima APP Dar es Salaam


Kampuni Sahara Sparks kesho inatarajia kuanza kongamano la vijana wabunifu litakalofanyika jijini Dar es Salaam ambalo limelenga kujadili namna gani ubunifu, teknolojia na ujasiriamali vinaweza kuwa ni chachu ya kuchangia maendeleo ya Tanzania.


Akizungumza na waandishi wa habari leo  jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa wiki ya Sahara Sparks, Mkurugenzi Mtendaji wa Sahara Ventures Jumanne Mtambalike, amesema kuwa wamekuwa wakiandaa tukio hilo kwa kipindi cha miaka saba  na kuwaleta pamoja vijana wenye mawazo yakiubunifu.


Aidha, amesema, wanategemea kufanya mijadala mingi sambamba na kuvumbua fursa nyingi kwa vijana kwa kushirikiana na wadau ambao ni pamoja na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Mradi wa Funguo na Clouds Media Group.


"Sahara Ventures ni kampuni tanzu ya Sahara Sparks ambayo inaandaa hili kongamano la vijana wabubifu lakini velevile ambao wanajiuhusisha na masuala ya teknolojia na ujasiriamali, pia inawaleta watunga sera kuweza kujadili mna gani ubunifu, teknolojia na ujasiriamali vinaweza vikawa ni chachu ya kuchangia maendeleo ya Tanzania kama Taifa"amesema Mtambalike.


Amesema wamekuwa wakifanya mijandala mbalimbali ambapo kwa mwaka huu kauli mbiu ni "Potantial Unleashed" kwamba namna gani wanaweza kufungua uwezo wa vijana kupitia teknolojia, ubunifu pamoja na ujasiriamali.


"Na kutakuwa na mijadala mbalimbali ambayo itaanza kesho tarehe 18 mpaka tarehe 21, 2022. Tutakuwa tunaangalia kwenye nyanja mbalimbali namna gani teknolojia na ubunifu vinatumika kwenye elimu, Afya, nishati na ajira," amesema Mtambalike.


Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH Dkt. Amos Nungu amesema wao kama wasimamizi wa masuala ya ubunifu, wanakila sababu ya kuhakikisha vijana wanapata fursa ya kuonekana, kubadilishana mawazo na kuweza kutangaza biashara zao.


"Ukweli ni kwamba vijana wana mawazo mazuri, kwahiyo kuwa na Jukwaa kama hili ni sehemu inayowapa fursa vijana kujitambua, kuwa pamoja na kuwa wabunifu lakini wanajua soko lina taka nini," amesema Dkt Amos.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI