Na Hamida Ramadhan Matukio Daima APP Dodoma
MKURUGENZI Mkuu Bohari ya Dawa MSD Mavere Tukai amesema kuwa bima ya afya kwa wote haiwezi kufanikiwa kama bidhaa ambazo ndio dawa zenyewe zitakuwa bei juu
Hata hivyo jukumu lao kama bohari ya dawa nikupambana kwa kutumia njia zote kuweza kupata bei shindani .
Aliyasema hayo leo jijini Dodoma wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mnyororo wa ugavi wa bidhaa za afya ambapo alisema kuwa “tunanunua kama wasemavyo wanunuzi kuwa value for money lakini sisi tunadhani siyo tu kwamba value for money bali kuwe na gharama nafuu ambayo itaweza kuhakikisha kwamba mifuko yetu ya bima inaweza kubeba,"
Na kuongeza kusema "kupimwa kipimo fulani na bima unayo unategemea kupata kile kipimo siyo unaambiwa nenda nje hivyo hapo pia MSD tuna deni la kuhakikisha kuwa tunapatikana katika maeneo yote kwahiyo tunatakiwa utekelezaji unapoanza na sisi tuwe tumesimama, " alisema.
Alisema kuwa katika kupunguza gharama za uagizaji wa bidhaa za Afya kutoka nje ya nchi itashirikiana na sekta nyingine ili kuwaimarisha na kuwanyanyua wazalishaji wa ndani ya nchi.
“Kwa sasa Bohari ya Dawa inaagiza zaidi ya asilimia 85 ya bidhaa za afya kutoka nje ya nchi hivyo kutumia gharama kubwa na wakati mwingine kuchelewa kupata bidhaa hizo kwa haraka”.
Mkurugenzi huyo alisema kuwa maboresho yanayofanyika kwa sasa ndani ya MSD yanalenga kutekeleza majukumu yake ya msingi ili kuendana na kasi kubwa ya uwekezaji wa serikali ya awamu ya sita katika sekta ya Afya.
“ Hivi sasa tuna vituo 7153 vya Serikali ambavyo vinasambaza Dawa nchini vipo kanda kumi za kimkakati pamoja na Dar es-Salaam, Mwanza, Dodoma, Kilimanjaro, Mtwara,Tabora kagera Mbeya,Iringa na Tanga.
Kwa upande wake Msemaji wa Serikali Gerson Msigwa alisema kuwa kwasasa bima ya afya kwa watanzania inawafikia kwa asilimia 15 tu na hivyo sheria ndio itawawezesha watanzania wote mtu anapoumwa aweze kutibiwa na kupatiwa dawa siyo habari za mgonjwa kaumwa inatakiwa mil.10 mnaanza kuchangishana au mnaanza kutafuta msamaha pengine nao haupatikani.
Msemaji huyo alisema kuwa lengo la serikali kila mtanzania akiumwa atibiwe kwa gharama yoyote ile,hivyo hilo ni jambo jema na siyo watanzania kuanza kuchangishwa hapana Bali uchangishwaji utawekwa katika utaratibu maalum .
“ Leo vikao vya kamati ya bunge vinaanza kamati yabunge inakuja kupokea maoni ya wadau,wadau watasema twendaje nahii sheria lakini niwahakikishie watanzania sheria hii ikipitishwa itakuwa bora na itatuondoa kwenye adha yakupata matibabu ambayo watanzania wengi wanayapata leo”alisema Msigwa.
Alisema kuwa Watanzania wengi watatibiwa mahali popote ,upatikanaji wa dawa,lakini kama fedha zakutosha hazipatikani ndio zitakusanywa kupitia utaratibu huo,na watanzania watachangia kulingana na uwezo wao,siyo kila mtu atapewa mzigo mkubwa,mapendekezo yatawekwa kwamba mtanzania mwenye uwezo wa chini au hali ya chini atachangia kulingana na hali yake.
“Lengo la serikali tunataka MSD tuwadai dawa siyo tuwadai dawa hatukuwapa pesa,kuna baadhi ya watu wanakuja wanapotosha watanzania , na mtu anazungumza kwasababu yeye ni mzima lakini wanasahau kuna watu kijijini wanashindwa kutibiwa kwasasbabu hawana pesa,kwahiyo ni jambo zuri na nchi nyingi zinafanya hivyo kuwa na bima ya afya kwa wote.






0 Comments