Header Ads Widget

MBARALI MGOGORO WA ARDHI WAPATA MUAROBAINI NA ELIMU YA MAZINGIRA KUTOLEWA



Jopo la mawaziri wa wizara 8 ikiwepo wizara ya Maliasili na utalii,TAMISEMI, wizara ya Ardhi na viongozi wengine Akiwepo mkuu wa mkoa wa Mbeya ndugu: Zuberi Homera leo hii wamewasili wilayani Mbarali mkoani ikiwa ni ziara ya kikazi kwa ajili ya kutafuta suluhu ya mgogoro wa Mpaka wa hifadhi ya Taifa ya Ruaha (RUNAPA) na vijiji vya wilaya ya mbarali. Lengo la ziara hiyo ni kujiridhisha na kutafuta suluhisho la kudumu juu ya malalamiko ambayo yamekuwa yakilalamikiwa na wananchi wa mbarali ambayo yalianza tangu lilipotolewa tangazo la serikali la 28 la mwaka 2008 GN 28


Katika ziara hiyo kamati imeweza kubaini na kushuhudia Uharibifu mkubwa wa mazingira hasa vyanzo vya maji unaotokana na Shughuli za kibinadamu, kupitia shughuli kama vile, kilimo,ufugaji na ukataji wa miti, jambo ambalo limekuwa likipoteza thamani na usalama wa mazingira ya hifadhi, kwani jambo hili linasababisha mvua kutonyesha na kukwamisha shughuli za kilimo, wanyama kutoweka, n.k,   Mh: Mary Francis Masanja amefafanua athari hizo akisema

kuna shughuli za kibinadamu nyingi zinafanyika ndani na maeneo jirani na hifadhi, ambazo kwa asilimia kubwa zinakinzana na shughuli za uhifadhi, Uhifadhi hauhitaji shughuli za kibinadamu ndani yake, ili maji yapatikane, ili umeme uwepo, ili mvua zinyeshe, lazima kuwepo na utulivu kwenye vyanzo vya maji, hivyo niwaombe sana hifadhi ni kwa ajili ya sisi binadamu na wanyama, hivyo tunajukumu la kuitunza, Uharibifu wa hifadhi unapofanyika ,tunapelekea kutoweka kwa wanyama, lakini pia muhimu kutambua hifadhi ni yetu wenyewe wahifadhi hawana faida yoyote na hifadhi isipokuwa sisi wenyewe. "Mary Masanja


Kupitia sakata hilo la utunzaji wa mazingira, muwakilishi kutoka wizara ya nishati aliweza kuelezea umuhimu wa vyanzo vya maji katika kuendesha mradi wa umeme nchini, na faida ya umeme nchini, hivyo wananchi wanakila sababu ya kutunza mazingira yao kwa maslahi mapana ya taifa.


Kupitia ziara hiyo naibu waziri wa TAMISEMI Mh: David Ernest Silinde alipata wasaa wa kutoa ufafanuzi mtambuka kuhusiana na mgogoro wa ardhi uliokuwa ukidumu kwa muda mrefu wilayani Mbarali, ambapo alianza kwa kusema:

 kuna makosa ambayo baadhi ya wenzetu katika ngazi za chini yalikuwa yanafanyika, na tunakiri kwamba makosa hayo yalikuwa yanafanyika, na kukiri kosa sio udhaifu bali ni kujifunza na kukubali kujirekebisha, na ndio maana sisi sote kwa pamoja tumekubaliana na serikali tutafanya usajili wa vijiji vipya, kwa kushirikiana na sekta zote, maana yake watu wa maliasili na utalii watatoa maoni yao, watu wa mazingira watatoa maoni yao, lengo ni kuondoa migogoro ambayo imekuwa haiishi kila mara, hatuwezi kuwa na migogoro ambayo haimnufaishi mtu yeyote, na ndio maana tukasema lazima tufanye hivyo ili kuondoa migogoro hii hapa mbarali, na hiyo ndio nia ya dhati ya serikali ya awamu ya sita kwa watu wa mbarali" David silinde




Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI