KAMATI ya Fedha na Utawala ya Halmashauri ya Mji Kibaha imekagua eneo ambalo lilivamiwa na wananchi na kupatiwa mradi wa upimaji viwanja 16,750.
Kamati hiyo ikiongozwa na mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Kibaha Musa Ndomba ilikagua eneo hilo linalounganisha mitaa ya Kidimu, Mkombozi na Lumumba imeridhishwa na mradi huo.
Kamati hiyo imeridhika na hali ya utekelezaji kwani tayari wataalam wameshapima Viwanja 12,066 kati ya Viwanja 16,750.
Akitoa taarifa Kaimu Mkuu wa Idara ya Mipangomiji na Ardhi Denis Festo amesema Kidimu vimepimwa Viwanja 4450,Mkombozi 6600 huku Lumumba vikipimwa Viwanja 1016 na kazi inaendelea.
Festo alisema kuwa tayari miundombinu ya ipo na inaendelea kuwekwa kwenye Maeneo yaliyosalia.
"Kamati imetoa rai kwa wananchi kuendelea na utaratibu wa kufika Ofisi za Halmashauri ili kupata gharama halisi ambazo kila mmoja atapaswa kulipia kutokana na Ukubwa wa eneo lake,"alisema Festo.
Aidha alisema kuwa zoezi hilo limeanza wiki mbili zilizopita
na ilikuwa liwe limeshakamilikahata hivyo kamati inaongeza wiki mbili nyingine kwa zoezi hilo baada ya hapo na viwanja vitawekwa sokoni kuwauzia wananchi wengine wenye uhitaji.
Halmashauri ya Mji Kibaha ilikopeshwa fedha kiasi cha shilingi 1.5 kutoka Wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa ajili ya utekelezaji wa Mradi wa kupanga,kupima na kumilikisha kwenye mitaa tajwa hapo juu kama mamlaka ya upangaji baada ya kupewa eneo hilo na Serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi.
0 Comments