NA TITUS MWOMBEKI Matukio Daima App Kagera.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Bukoba Hamid Njovu amesema kuwa yalifanyika mabadiliko ya kanuni katika utoaji wa mikopo ya 2% inayotolewa kwa watu wenye ulemavu, katika mabadiliko hayo yanamruhusu hata mtu mmoja kupatiwa mkopo.
Ameyasema hayo katika mahojiano maalumu na Matukio Daima ofisini kwake na kusisitiza kuwa mabadiliko hayo yametokana na uchache wa kundi la watu wenye ulemavu katika jamii ukilinganisha na makundi mengine yanayonufaika na mikopo itolewayo na halmashauri.
“Tumeweza kufanya mabadiliko katika kanuni na mabadiliko katika utowaji wa mikopo ya 2% inayotolewa na halmashauri kwa kundi la watu wenye ulemavu ambapo kutokana na uchache wa kundi hili katika jamii zetu hapa hata mtu mmoja mwenye ulemavu anaweza kuja hapa akajaza taarifa zake na kupatiwa mkopo” alisema Njovu
Ameongeza kuwa nje na kisheria kuruhusu watu wenye ulemavu halmashauri ya Manispaa ya Bukoba katika mwaka 2021/2022 waliweza kutenga zaidi ya milioni 44 kwaajiri ya kuwakopesha watu wenye ulemavu lakini idadi ya vikundi vilivyojitokeza kupatiwa mikopo ni vikundi vitano tu.
“Unaweza kushangaa nje na sharia kuwaruhusu mtu mmoja au kuunda kikunmdi cha watu wawili bado mhitikio ni mdogo na labda ni kutokana na uchache wao tunawatengea asilimia zao lakini wanaojitokeza kuomba ni wachache kwa mfano katika mwaka 2021/2022 vimejitokeza vikundi vitano tu vilivyojikopa mil.22 tu”
Kwa upande wake Afisa Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Bukoba, Murshid Issa amebainisha vigezo vinavyotakiwa kwa kundi la watu wenye ulemavu ni vya kawaida na huku akitaja changamoto mbalimbali wanazopitia katika kufanikisha utowaji wa mikopo katika kundi hili ikiwemo watu wenye ulemavu kushindwa kufanya marejesho.
“kwa kundi hili hata mtu mmoja anaweza kuomba mkopo kwa kigezo atatambulishwa kuwa ni mmoja huyo hana haja ya kuwa na katiba ni utambulisho tu kutoka katika serikali ya mtaa na kujaza vinavyotakiwa tu, lakini kama ni kikundi mnatakiwa kuwa na katiba, utambulisho kutoka kwa viongozi wa serikali ya mtaa au ya kata, mhutasali wa usajili kuwa wanakikundi wamekubaliana, azimio la kuanzisha kikundi hii tunatoa hapa ofisini tunawapa wanaenda kuijaza, orodha ya wanakikundi na hapa kila mwananchama”
“Kundi hili limekuwa likifanya vibaya katika marejesho ukilinganisha na makundi mengine huku wengine wakisema kuwa mtu mwenye ulemavu huwezi kumkopesha bali unamsaidia suala ambalo sio kweli kwani hii sio ruzuku ni mkopo, ukiangalia walio jikopa mwaka 2019/2020 vilijikopa vikundi vitano lakini hakuna kikundi kilichomaliza kulipa mikopo yao”
Amesisitiza kuwa watu wenye ulemavu katika Manispaa ya Bukoba waendelee kuomba mikopo kwani fedha zipo kwaajiri yao, serikali imetenga fedha hizo ili kuwasaidia kujikwamua kiuchumi kupitia kodi za wananchi na waelewe kuwa serikali inapoamua kuwakopesha nao wakaweza kufanya shughuli za uzalishaji wakumbuke kufanya marejesho ili na wengine waweze kunufaika.
Kwa upande wake Juma khamis ambaye ni mlemavu wa viungo anayeishi mtaa wa Mchangani kata ya Kibeta Manispaa ya Bukoba amesema kuwa watu wenye ulemavu wanatamani sana kuomba mikopo hiyo lakini wengi wao bado hawana elimu ya kutosha hasa namna ya kuweza kupata mikopo hiyo huku akiwaomba viongozi wa Manispaa ya Bukoba kuendekea kutoa elimu ya kutosha hata kupitia kwa viongozi wao wa Shirikisho la Vyama Vya Watu Wenye Ulemavu (SHIVYAWATA).
0 Comments