Na Amon Mtega,Mbinga.
JUMUIYA ya umoja wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi CCM (UWT) Wilaya ya Mbinga Mkoani Ruvuma imetuma salamu kwenye chaguzi zinazoendelea kuwa ndani ya CCM na Jumuiya zake kuwa wamejipanga kuwachagua Viongozi imara watakaokiongoza Chama hicho na Jumuiya zake bila upendeleo.
Kauli hiyo imesikika kwa baadhi ya Wajumbe wa uchaguzi wa UWT Mbinga baada ya kuupata uongozi mpya ambao utakaoongoza Jumuiya hiyo kwa muda wa miaka mitano ambapo kwa nafasi ya kiti ameibuka mshindi Grence Milinga(Madeleke)kwa kura 465 aliyemfuatia Consolata Haule ambaye alikuwa anatetea nafasi yake amepata kura 138 huku Victoria Milinga amepata kura 58 na Wajumbe walikuwa 665 toka kata 48 kura tisa zimeharibika.
Wajumbe hao wakati wakishangilia ushindi huo wamesema kuwa kazi imeanza ya kuhakikisha wanapatikana Viongozi wasiyowagawanya wanachama kwa maslai yao binafsi na ambao watakao msaidia Mwenyekiti wa CCM Taifa ambaye pia ni Rais wa Tanzania mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ambaye wakinamama hao wamempongeza kwa kazi kubwa anayoifanya.
Wapigakura hao ambao baadhi yao wametumia usafiri wa kujitegemea kutoka Vijijini wamesema wametumia garama zao ili kutimiza demokrasia ya kuwa na haki ya kumchagua kiongozi wanayemtaka huku wakiwapongeza makatibu wa Jumuiya zote wa Wilaya hiyo pamoja na katibu wa CCM Wilayani Mbinga kuwa wamesimamia chaguzi hizo kwa haki .
Katika uchaguzi huo Viongozi wa nafasi mbalimbali ikiwemo ya Halmashauri kuu na mkutano mkuu wa CCM ambapo Oresta Mbunda aliibuka kuwa mshindi wa kura 349 aliyemfuatia Dokela Christian kura 244 huku mgombea wa tatu Felisiana Haule kura 67.
Kwa upande wake katibu wa Jumuiya hiyo Elimina Makiya amesema kuwa uchaguzi huo umezingatia taratibu zote na kuwa ameshaupokea uongozi mpya ambao ataendelea kufanyanao kazi ya kuipeleka mbele Jumuiya hiyo.
Naye mwenyekiti mpya Grence Milinga(Madeleke) amewashukuru Wajumbe hao huku akiwaahidi kufanyanao kazi kwa karibu zaidi ili kuzibaini changamoto zinazowakabili na kuzitatua kwa pamoja.
0 Comments