Teddy Kilanga, Arusha
Watendaji wa mahakama kutoka nchi za ukanda wa Afrika wametakiwa kuzingatia uhuru wa vyombo vya habari na usalama wao katika utoaji wa sheria na misingi yake kwa lengo la kuhakikisha waandishi wa habari wanauhuru wa kutoa habari.
Akizungumza kando ya mafunzo ya watendaji wa mahakama juu ya uhuru wa kujieleza na usalama wa waandishi wa wanahabari yaliyoandaliwa na shirika la elimu,sayansi na utamaduni la umoja wa mataifa(Unesco) ,Rais wa mahakama ya Afrika ya haki za binadamu na watu,Jaji Imani Abudi alisema lengo ni kuhakikisha waandishi wa habari wanayo haki ya kuandika habari pamoja na kusikilizwa.
"Uhuru wa vyombo vya habari na usalama wao ni jambo muhimu sana kwani waandishi wa habari ni watu muhimu katika jamii yoyote ambayo inaheshimu juu ya utawala wa sheria,demokrasia na haki za kibinadamu,"alisema Jaji Abudi.
Alisema kupitia mafunzo hayo yatasaidia kupata elimu namna vyombo vya utoaji haki kutoka Afrika vinaweza kutumika kwa njia bora ya kuweza kuhakikisha kwamba waandishi wa habari wanakuwa na uhuru wa kutoa na kupewa habari pamoja na kusikilizwa kwa kuzingatia usalama wao.
"Pia Majaji watafundishwa namna njema ya kushughulikia mashauri yanayohusu wanahabari kwa kuzingatia misingi ya sheria za nchi mbalimbali zilizopo Afrika hivyo nasisitiza kuwa namna mahakama ya haki za kibinadamu na wanatu inavyotoa maamuzi yake mbalimbali,"alisema Rais huyo.
Alisisitiza kuwa mahakama za nchi katika umoja wa Afrika wanaweza kushirikiana katika kubadilishana uzoefu kwenye maamuzi na mambo mengine yanahusiana na masuala ya wanahabari pamoja na haki zao.
Aidha alisema ni vyema wanahabari wa nchi za Afrika wakawa wazalendo katika kulipoti matukio mbalimbali yanayohusu bara la Afrika ili kudumisha amani kuepuka kwa kuzingatia usalama wao.
Kwa upande wake Rais wa mahakama ya jumuiya ya Afrika ya mashariki(EACJ), Nestory Kayobera alisema katika kipindicha miaka 20 wameshapokea kesi mbalimbali zaidia ya 170 ambapo kila mwananchi kutoka nchi mwananchama anahaki ya kufungua kesi bila masharti yoyote.
Naye David Ngunyale ni mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo alisema mafunzo hayo ni muhimu kwao katika kujengewa uelewa kwani kwa kushindwa kufanya hivyo itawapelekea kushindwa kufanya kazi na watu wengine wakiwemo waandishi wa habari.
"Kwa hiyo kwa msingi mkubwa wa mafunzo haya ni kwa ajili ya utawala wa sheria unavyohusianishwa na uhuru wa kutoa habari,"alisema.
Mkuu wa mradi wa uwajibikaji wa wanahabari kutoka UNESCO Mehdi Benchelah alisema kuwa uhuru wa kujieleza imekuwa ni changamoto kubwa Duniani ambapo kumekuwa na kesi nyingi za wanahabari wakati mwingine wanauwa jambo linaloathiri tasnia nzima ya habari na wananchi kwa ujumla kwa kukosa uhuru wa kupata habari.
"UNESCO tumeona ni vyema kuwapa mafunzo haya watendaji wa mahakama ili kuwapa uelewa juu ya utawala wa kisheria na uhuru wa kujieleza ambapo wanapadishana mawazo ni vipi nchi za ulaya na za Afrika zinavyofanya katika kuhakikisha uhuru wa habari unakuwepo na kuweza kusimamia suala hili,"alisema Benchelah.
Mmoja wa wanahabari aliyehudhuria mafunzo hayo,Lucas Miyovela alisema ni vyema wadau hao wakaanza kuwashirikisha waandishi wa habari moja kwa moja ili waweze kufahamu changamoto zinazowakabili.
0 Comments