Header Ads Widget

ALIYEMZUSHIA KIFO DKT MWAKYEMBE AFIKISHWA MAHAKAMANI

TARZAN  Mwambengo (27), mkazi wa Ukonga jijini Dar es Salaam,mzaliwa wa mkoa wa Mbeya aliyemzushia kifo waziri mstaafu Dk. Harrison Mwakyembe na kuutangaza msiba huo kwa siku kadhaa na baadaye kurusha matangazo ya mazishi ya kiongozi huyo nyumbani kwake Kyela, amekamatwa na Jeshi la Polisi na kufikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Mwambengo, mkazi wa Ukonga jijini  alifikishwa katika mahakamani hiyo juzi Jumatatu tarehe 26 Septemba, 2022 kujibu mashtaka ya kusambaza taarifa za uongo mtandaoni.

Mtuhumiwa huyo anadaiwa kutenda makosa hayo ya kimtandao kuanzia tarehe 9 Agosti, 2022 hadi 12 Agosti, 2022 kupitia luninga yake ya mtandaoni iitwayo Kalomba Tv yenye wafuatiliaji (subscribers) 221,000


Akisomewa mashtaka matano ya kutenda makosa ya kimtandao mbele ya Hakimu Mkazi Mheshimiwa Kabate, mshtakiwa hakukiri makosa hayo.

Mshtakiwa Tarzan Mwambengo baada ya kukana mashtaka hayo aliachiwa huru kwa dhamana hadi 24 Oktoba, 2022 wakati kesi hii iliyopewa namba 138/2022 itapokuja tena kwa kusikilizwa.

Taarifa hizo feki za kifo cha waziri na mbunge mstaafu wa Kyela, ziliwashtua watu wengi ndani na nje ya nchi kwani Dk. Mwakyembe mbali na kuitumikia serikali katika wizara tano tofauti (Ujenzi, Uchukuzi, Afrika Mashariki, Katiba & Sheria na Habari, Utamaduni, Sanaa & Michezo), alikuwa mbunge machachari wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mbunge wa bunge la Afrika Mashariki, mhadhiri mwandamizi wa sheria Chuo Kikuu cha Dar-es-salaam na wakili wa kujitegemea wa Mahakama Kuu ya Tanzania.

Aidha,picha zilizorushwa na KALOMBA TV, zilionyesha viongozi kadhaa wakilia akiwemo Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kasim Majaliwa na mke wake Mheshimiwa Mary Majaliwa na mbunge wa Simanjiro Mheshimiwa Christopher Ole Sendeka ambaye ni rafiki mkubwa wa Dk. Mwakyembe, na kuzifanya taarifa hizo kubeba ushawishi mkubwa wa kuaminika.(chanzo Singidaniblog)

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI