Mkurugenzi wa Utafiti na Ubunifu wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) Dkt Joseph Ndunguru pamoja na mtafiti kutoka TARI Uyole Ndugu Frank Ratego wanatembelea vikundi, makampuni na wakulima wanaozalisha miche ya parachichi katika mikoa ya Mbeya, Njombe na Iringa ambao wamepatiwa mafunzo na vyeti na TOSCI.
Madhumuni ya ziara hiyo ni kuchagua vikundi au makampuni ambayo yanaweza kushirikiana na TARI katika kuzalisha miche ya palachichi na kufikia malengo yake ya mwaka 2022/2023.
Baadhi ya Makampuni na vikundi vilivyotembelewa ni pamoja na Kamouni ya Kuza iliyopo Rungwe Mbeya, kikundi cha Palachichi Kwanza (Mbeya Jiji), Nemes Green Farm (Njombe), Kampuni ya Hamlun (Njombe), Kampuni ya MADEBE (Njombe), AgriPromise (Njombe) na Sadalate Green Gold Garden
0 Comments